Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation imetoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya kupikia kwa baadhi ya koo za Kimasai wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Wafanyakazi wa Oryx Gas wakiongozwa na Meneja wa Masoko wa kampuni hiyo Peter Ndomba kwa kushirikiana na Doris Mollel foundation wamefika katika nyumba za koo za Kimasai na kuwafundisha matumizi salama ya nishati ya gesi.
"Tunafahamu jukumu ambalo tunalo kama kampuni ni kuendelea kutoa elimu ya matumizi salama ya majiko ya gesi, tumefanya hivyo katika makundi mbalimbali katika jamii ya Watanzania na leo hii kwa kipekee mafunzo haya tunayoa kwa koo hizi za Kimasai na tumetumia nafasi hii kuwapa elimu na kuwagawia bure mitungi ya gesi na majiko yake."
Akieleza zaidi Ndomba amesema wanamshukuru Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel kwa jitihada zake za kuwafikisha Oryx katika boma za koo za Kimasai na kutoa elimu hiyo.
Amesisitiza Oryx itaendelea na mkakati huo kwa koo nyingine zaidi ili jamii yote ya Watanzania iweze kutumia nishati hiyo safi na bora kwa mapishi na kwamba utoa huo elimu pia umeenda sambamba na ugawaji mitungi ya gesi 300 kwa kada ya watumishi wa sekta ya afya wilayani Siha.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...