NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MWANZA
MAJAJI
wa Mahakama Kuu Kanda ya Ziwa na Wakurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi
(CMA) wameanza kikao kazi kilichoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
ili kuwajengea uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Kifungu cha 5 (Sura
263 marejeo ya mwaka 2015).
Kikao
hicho kilichofunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF), Dkt. John Mduma, Septemba 15, 2023, jijini Mwanza, kinafuatiwa na kikao
kama hicho kilichofanyika Juni 9, 2023 mjini Bagamoyo na kuhudhuriwa na Majaji
wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, kutoka Kanda ya Dar es Salaam na Pwani,
pamoja na wakurugenzi wa CMA.
Akizungumza
na washiriki hao, Dkt. Mduma amesema, Mahakama ni chombo muhimu katika mchakato
wa ulipaji wa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na
kazi walizoajiriwa kwa mujibu wa mkataba
Amesema,
mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita
chini ya uongozi mahiri wa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ya kuzitaka taasisi za umma kuongeza ufanisi na ubora wa utoaji
huduma kwa wananchi.
“Kwa hivyo Mahakama na
CMA ni wadau muhimu katika utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi
lakini pia tunajenga uelewa wa pamoja, kikao kazi hiki, kitaleta manufaa
makubwa ikiwemo kuimarisha mahusiano, kwa lengo la kutoa huduma bora kwa
wananchi na kuchangia kwenye kukuza uchumi wa nchi yetu.” Alifafanua Dkt.
Mduma.
Kwa
upande wake Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt.
Yose Joseph Mlyambina ameipongeza Menejimenti ya WCF kwa kuwa tayari kushirikiana
na Mahakama pamoja na taasisi zinazohusu utatuzi wa migogoro ya kazi katika eneo la kujenha uelewa wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.
Alisema,
mafunzo hayo yatasaidia sana taasisi hizo kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya
sheria zinazohusu ulipaji wa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia au kuugua wakiwa
kazini au kwa familia za wafanyakazi wanaofariki kutokana na ajali wakiwa
kwenye ameneo yao ya kazi.
“Mheshimiwa
Jaji Mkuu alifanya ugatuzi kwa kuelekeza Waheshimiwa Majaji wote wa Mahakama
Kuu ya Tanzania Manaibu Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wote, kwa sehemu ambazo hazina Masjala ya za Mahakama Kuu kushughulikia mashauri ya Kazi,
hivyo niliwaomba WCF watuandalie mafunzo mengine ya kikanda na nashukuru leo tuko hapa Mwanza.”
Kaimu
Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA, Bw. Thomas Malekela, alisema
tume inashughulikia haki zilizovunjwa mahali pa kazi.
“Mfanyakazi
anaweza akalalamika juu ya mshahara ambao kwaweli si wenyewe, anazungumzia
mshahara pamoja na mamslahi, CMA ikitoa uamuzi kuwa mshahara wako halisi ni
huu na ndio utakaozingatiwa, WCF itatumia uamuzi huo wa CMA katika kutekeleza jukumu lake la kulipa
fidia.” Alifafanua Bw. Malekela.
Pamoja
na kujifunza sheria ya fidia kwa wafanyakazi, maeneo mengine ambayo Majaji hao
pamoja na wakurugenzi wa CMA wamejifunza ni taratibu za Madai ambapo wamepata
fursa ya kuelezwa jinsi tathmini za madhara ambayo mfanyakazi ameyapata
zinavyofanyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...