Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiwa katika kikao kazi na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo Septemba 26, 2023.

Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu dira na muelekeo wa utekelezaji wa majukumu na shughuli mbalimbali za kila siku za Wizara katika kuwahudumia wananchi na kutimiza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wengine walioshiriki katika kikao kazi hicho ni Naibu Katibu Mkuu (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi na Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), Bi. Agnes Meena.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...