BANK OF AFRICA Tanzania, inaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ikiwa na nia ya kuweka mkazo katika kufanikisha dhamira yake inayolenga kutoa umuhimu wa kwanza kwa mteja katika kutoa huduma zake. Ikiwa chini ya Benki ya kimataifa yenye mtandao barani Afrika inatambua jukumu muhimu linalofanywa na wafanyakazi wake katika kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na uzoefu wa wateja vinafikiwa katika matawi yake yote nchini. Benki iko thabiti katika kujitolea kusikiliza mahitaji ya wateja wake na ushirikiana kuyapatia ufumbuzi ikisaidia programu za kutoa huduma bora zinazotekelezwa za mtandao mzima na matawi ya benki yaliyopo chini ya Benki mama ya BMCE BANK OF AFRICA

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho haya jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Bw. Adam Mihayo ametoa pongezi kwa Wafanyakazi wa Benki hiyo kwa kusema “Tunasherehekea wiki hii kwa kauli mbiu ya “Timu thabiti ya Huduma” inayohimiza kufanya kazi kwa ushirikiano kuanzia wafanyakazi wanaouhudumia wateja na wale ambao kazi zao hawakutani na wateja moja kwa moja, tunaungana kukuza utaalamu, nidhamu, mazingira rafiki na kutoa huduma bora kwa kuzingatia maadili, kurahisisha huduma na kuhakikisha zinapatikana haraka".

"Siku zote katika wiki hii kila mwaka, tunaitumia kuwashukuru wafanyakazi wetu kwa kujitolea kutoa huduma bora kwa wateja kwendana na mabadiliko yanayojitokeza kila siku katika sekta ya kibenki. Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha inabadilika kwa kasi duniani na Tanzania iko mstari wa mbele kwendana na mabadiliko haya. Miaka michache iliyopita, hakukuwa na huduma nzuri za Mawasiliano; huduma za benki zilipatikana sehemu maalum na sio kwa wakati wowote, Kwa sasa huduma hizi zinapatikana kupitia njia mbalimbali kiasi kwamba kwendana na mabadiliko haya inapaswa kuelewa matakwa ya wateja sambamba na kuwa na ubunifu wa bidhaa/huduma zinazowarahisishia maisha na biashara zao.Ili Kuweza kuhimili mabadiliko haya ni muhimu kuelewa matakwa ya wateja na kwendana nayo kwa kuungana nao,kuwa na taarifa,kuwezeshwa na sisi kama Benki tunayazingatia.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yanayoadhimishwa kila mwaka hutumiwa kupata maoni ya wateja kuhusiana na huduma zinazotolewa na Benki na changamoto zanazowakabili kibiashara ili kutafuta njia za kibunifu za kuyashughulikia. Kama benki inayojali wateja, BANK OF AFRICA kwa miaka mingi imetumia maadhimisho haya kuweka mkazo katika utoaji huduma bora kwa wateja kama kipengele muhimu cha maadili yake ya msingi na pia kutoa shukrani kwa wateja kwa kuendelea kuiamini na kuendelea kufanya nayo biashara.

Katika kuelewa umuhimu wa ushirikishwaji wa kifedha na kuboresha uzoefu wetu kwa wateja, benki imefanya uwekezaji ili kuboresha mifumo yake ya kidijitali ikijumuisha huduma za benki kwa njia ya simu - B-Mobile, na matumizi ya huduma kwa njia ya mtandao - ya BOAWeb inayosaidia kujenga jamii inayoweza kupata huduma mbalimbali bila kulazimika kutumia pesa taslimu. Uboreshaji wa programu ya mashine za kutolea fedha (ATM) na njia nyinginezo za kidigitali zinazowarahisishia wateja wake maisha ikiwemo huduma mpya ya Bank of Africa WAKALA iliyozinduliwa karibuni yenye mtandao wa mawakala zaidi ya 100 kwa lengo la kuwafikishia wateja huduma wa benki karibu zaidi.
Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania, Adamu Mihayo (katikati ) akikata utepe kuashiria uzindzui wa wiki ya huduma kwa wateja wakati wa hafla iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wanaoongoza vitengombalimbali katika benki ya BOA Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania, Adamu Mihayo (katikati ) na Maofisa Waandamizi wa Benki hiyo wakionyesha ujumbe wa wiki ya huduma kwa wateja kwa waandishi wa habari
Mkurugenzi Mkuu na Afisa  Mtendaji Mkuu wa Bank Of Africa (BOA) Adamu Mihayo (kulia ) akimkabidhi keki mmoja wa wateja wa benki hiyo Harrison Moses wakati wa hafla ya uzinduziwa wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam,
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja na Ubora wa Bank of Africa Tanzania, Bibi Anna Roberta Mango,akiongea na wafanyakazi wa Benki hiyo wakati wa maadhimisho hayo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bank Of Africa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...