Na Shalua Mpanda -TMC


MKUU wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Sixtus Mapunda ametoa mwito kwa wadau wa elimu nchini kutumia changamoto iliyopo ya upungufu wa walimu kubuni mbinu za kisasa kukabiliana na changamoto hiyo.

Ametoa mwito huo wakati wa sherehe za mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kijichi ambapo amesema Serikali inajitahidi kuajiri walimu  lakini haiwezi kumaliza changamoto hii hivyo ni  wakati muafaka sasa kuanza kutumia teknolojia kukabiliana na jambo hili.

"Tumieni walimu wachache waliopo lakini kwa mfumo wa kisasa,Dunia hivi Sasa mwalimu anaweza kuwa darasani lakini akamfundisha mtoto akiwa hapa...kinachotakiwa hapa ni 'internet' na  screen kubwa, " amesema Mapunda.

Katika hatua nyingine Mapunda amewashukuru walimu wanaojitolea katika Shule hiyo ambapo ameahidi kukutana na walimu hao ofisini kwake kuzungumza nao kama motisha kwa kazi wanayofanya.

Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa ikiipa kipaumbele sekta ya elimu kwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha miundombinu ya elimu

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya,Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Catherine Mdachi amesema wamejipanga kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne mwaka huu kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na walimu.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...