Bunge la Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wamesaini Andiko la Mradi wa Awamu ya Tatu wa Kuwajengea uwezo Waheshimwa Wabunge na Watumishi wa Bunge (LSP III) wenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00. Aidha, Mradi huo utahudumia pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Andiko hilo limesainiwa leo tarehe 11 Oktoba, 2023 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam ambapo Utekelezaji wa Mradi huo utaanza Mwezi Oktoba 2023 hadi Novemba 2027.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Ndg. Sergio Valdini wakisaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi akishuhudia tukio hilo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndg. Sergio Valdini katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Oktoba, 2023
.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Ndg. Sergio Valdini wakisaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi akishuhudia tukio hilo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akibadilishana hati na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Ndg. Sergio Valdini mara baaada ya kusaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...