Na Muhidin Amri,Tanganyika


MKUU wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Onesmo Busweru,amewataka wananchi wilayani humo kutunza na kulinda vyanzo vya maji ili miradi ya maji inayojengwa iweze kudumu kwa na kuendelea kuwaondolea adha ya upatikanaji wa maji katika maeneo yao.


Busweru ametoa agizo hilo jana,wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Majalila Halmashauri ya wilaya Tanganyika baada ya kukagua mradi wa maji uliotekelezwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa).


Alisema,maji ni rasimali adhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai wengine na haina mbadala wake,hivyo wananchi wanapaswa kuvilinda vyanzo,miradi ya maji,miundombinu na mazingira ili kuepuka kutokea ukame unaoweza kusababisha vyanzo vyanzo vya maji kukauka.


Alisema, mradi wa maji Majalila ni umekuja kwa muda muafaka kwani umeleta suluhu ya changamoto ya huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa eneo hilo ambao kwa muda mrefu hawakuwa na maji uhakika,badala yake walitegemea visima vya asili kupata maji kwa matumizi yao ambayo hayakuwa safi na salama.


Busweru,amewaagiza viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani humo,kuhakikisha wanatumia sheria,taratibu na kanuni zinazosimamia masuala ya maji kama vile kutofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo.


Amewataka wananchi wa Tanganyika kutunza mazingira,kuacha kukata miti ovyo na kuchoma moto misitu na kulinda miundombinu ya maji kwani serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza na kufikisha huduma ya maji kwa manufaa yao.


Aidha Busweru,ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wawataalam wa Ruwasa ngazi ya wilaya na mkoa wa Katavi kwa kuendelea kutekeleza na kusimamia vizuri miradi ya maji wilayani Tanganyika.


Alisema,mradi huo na miradi mingine iliyotekelezwa imewawezesha wananchi kupata maji safi na salama na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi badala ya kutumia muda wao kwenda kutafuta huduma ya maji mbali na makazi yao.


Mkazi wa kijiji hicho Neema Joseph,ameishukuru serikali kwa kutekeleza na kuwaleta mradi huo kwani umewasaidia kupata huduma ya maji safi na salama kwenye maeneo yao na hivyo kutoa fursa kwao kutumia muda mwingi kujikita katika shughuli za maendeleo.


Alisema,amelazimika kuingiza maji ndani ya nyumba yao ili kuepuka kero ya kubeba maji kichwani yanayopatikana mbali na makazi na kuwataka wananchi wengine kuvuta maji majumbani ili kuepuka adha ya kukaa kwa muda mrefu kwenye vituo vya kuchotea maji.


Rebeca Ngangu alisema,kabla ya mradi huo kujengwa walikuwa wanatumia maji ya visima vilivyochimbwa na mikono ambayo hayakuwa safi na salama,kwa kuwa hawakuwa na njia mbadala ili kuokoa maisha yao na mifugo.


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Majalila wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,wakichota maji katika moja ya vituo maalum vya kuchotea maji vilivyojengwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Ruwasa kupita mradi wa maji Majalila,kulia anayeangali koki mkuu wa wilaya hiyo
Onesmo Busweru.

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Onesmo Busweru kulia,akimtiwsha ndoo ya maji mkazi wa kitongoji cha Kawambwe kata ya Majalila Neema Tumba,baada ya kukagua mradi wa maji uliotekelezwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa). 

Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Kawambwe kata ya Majalila wilaya ya Tanganyika wakimsikiliza mkuu wa wilaya  hiyo Onesmo Busweru kulia, baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa maji Majalila ambapo amewataka wakazi hao kuhakikisha wanatunza vyanzo  na kulinda miradi ya maji ili iweze kuwa endelevu na kudumu kwa muda mrefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...