Na. Damian Kunambi, Njombe
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Caludia Kitta amewataka viongozi wa sekta ya elimu pamoja na viongozi wa dini wilayani humo kuhakikisha watoto wanajifunza mila na desturi za kitanzania na kupewa kipaumbele ili kuepusha watoto hao kujifunza tamaduni zilizo potofu na hasa za mataifa ya Magharibi.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa Rai hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya sekondari Elly's iliyopo katika kata ya Ilembila wilayani humo na kuhusisha viongozi wa kidiasa, wataalam mbalimbali, wazazi pamoja na wadau wa elimu wa wilaya hiyo.
Yohana Gwihaya ni mwalimu wa shule ya sekondari Elly's na Yaledi Mlyuka ni mdau wa maendeleo ya elimu wilayani humo wamesema kuwa watoto wanapolelewa katika misingi ya kiimani na kiroho husaidia kuwa na maadili yaliyo mazuri kwakuwa wanakuwa na hofu ya Mungu.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wazazi walio huzuria mkutano huo wamesema kwa karne ya watoto wamekuwa wakiharibika na kuharibiwa na walezi wasio waaminifu hivyo ni vyema kujenga utaratibu wa kuzungumza na watoto mara kwa mara pamoja na kuwaasa kuwa na maadili yaliyo mema.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...