Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Kudhibiti  na Kupambana na Dawa za Kulevya  Kanda ya Kaskazini imeteketeza viroba  vya bangi kavu  237 na mbegu za bangi zenye uzito wa kilogramu 310 iliyokuwa tayari kwa kupandwa

Akizungumza katika zoezi la kuteketeza bangi hizo dampo la  Kikatiti Wilayani Arumeru,mkoani Arusha , Mkuu wa Operesheni wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini  ,Innocent Masangula  amesema bangi hizo zilikamatwa katika operesheni maalum.

Amesema mifuko hiyo iliyopo kwenye viroba hivyo imekamatwa kutokana na operesheni maalum iliyofanyika maeneo mbalimbali eneo husika linalolima bangi  wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Emanuela Kaganda

"Operesheni bado itazidi kuendelea ikiwemo utoaji elimu juu ya ulimaji zao mbadala lakini hatulali tutaendelea kupambana na dawa haya"

Ambapo DC Kaganda alisema bangi hizo zimeteketezwa eneo hilo na katika kipindi cha Septemba gunia 90 za bangi zilikamatwa Oktoba mwaka huu, gunia 225 na kupelekea jumla kuwa gunia 316 sanjari na kilo 310 za bangi.

"Gunia nyingine tumeziteketezwa shambani nyingine zimeteketezwa hapa,na tutaendelea na zoezi hili"

Ameongeza kuwa  serikali imejipanga kutoa elimu juu ya dawa ya kulevya ikiwemo ulimaji wa  zao mbadala ili waachane na madawa hayo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...