Na Mwandishi Wetu
MLEZI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata za Makongo, Kinondoni na Bunju, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambaye ni Diwani wa Viti Maaumu, Grace Mwashala, amekabidhi msaada wa wa vitu mbalimbali vyenye thamani y ash. 1,200,000 kwa uongozi wa UWT Kata ya Kinondoni, jijinii Dar es Salaam.
Diwani huyo amekabidhi vitenge 55,kadi za UWT 333 , fedha ya kufungua akauti 20,000 na fedha za kuanzia akiba katika akaunti sh. 50,000.
Grace amesema dhamira ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwakwamua wanawake kiuchumi kwani vitu hivyo alivyo kabidhi ni kwaajili ya kuanzisha mradi ambapo fedha itakayopatikana itaingizwa katika akauti ya UWT ya kata hiyo.
MLEZI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata za Bunju, Makongo na Kinondoni ambaye pia ni Diwani wa Viti Malumu, Grace Mwashala (katikati) akikamkabidhi Katibu wa umoja huo Kata ya Kinondoni Asia Aliy msaada wa vitenge kwaajili ya kuanzisha mradi wa UWT Kata, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wa Kata hiyo Bupe Mwakyangi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...