NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Benki ya Equity imezindua huduma mpya katika kituo cha huduma kwa wateja iitwayo LIVE CHAT ambayo ni kidigitali inayomuwezesha mteja kupata huduma muda wowote kwa masaa 24 kwa mwaka mzima.

Akizungumza leo Oktoba 4,2023 na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya EQUITY, Isabela Maganga amesema kuwa huduma hiyo imewasogeza karibu zaidi na wateja na itamfanya mteja kuweza kuwasiliana na mtoa huduma wa Benki moja kwa moja Live na kuweza kupata huduma hapo hapo.

"Huduma ya Live Chat faida yake kubwa ni kutuweka sisi karibu sana na wateja wetu ambapo mteja na mtoa huduma wanaongea Moja kwa moja Live na kuweza kumpa huduma hapo hapo" Amesema Bi.Isabela

Aidha Bi.Isabela amesema Kupitia huduma hiyo, mteja atapata faida ya kurahisisha muda wake wa kutosubiri kupata huduma kwa muda mrefu ambapo akishaingia hewani mteja anakutana na mtoa huduma hapo hapo.

"Mteja anapata ujuzi wa tofauti na kupiga simu, mteja akipiga simu huwa anakaa kidogo anasubiri mpaka mtoa huduma apokee lakini Live chat yenyewe haina kusubiri akiingia online anamkuta tayari mtoa huduma yupo , wanaongea, anatatua na anampa solution Moja kwa moja" Alisema Maganga na kuongeza kuwa

"Hii inasaidia sanasana kwa wale ambao Wana simu janja katika kufanya mawasiliano kidigitali na kutumia huduma za kibenki papo kwa papo"

Kadhalika Maganga amesema Benki ya EQUITY imewekeza kwenye njia nyingi sana za kimtandao za kidigitali, ambapo mpaka sasa asilimia 88 ya wateja wao wanahudumiwa kwa mifumo ya kidigitali kwa kutumia simu za mikononi, Kompyuta lakini pia kwa kutumia website.

"Mteja akiwa na simu yake ndiyo Benki yake, akiwa na kompyuta yake ndiyo Benki yake, akiingia kwenye mtandao wowote anakutana na Benki yake na Benki yake ni EQUITY"

Pamoja na hayo amesema Kituo cha huduma kwa wateja wanazidi kukipanua na kuongeza huduma zaidi ili waendelee kuwa karibu zaidi na wateja wao na kuendelea kutoa huduma kwa muda wote asubuhi mpaka usiku.

"Nawakaribisha sana wateja wetu Equity na pia nawashurku kwa kutuamini sisi ambao tunawapa huduma za kibenki na pale tunapokua tunatimiza malengo yao ya shughuli zao za kiuchumi na kijamii"

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Equity Tawi la Mwenge, Magreth Makundi ameahidi kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa kiwango Cha juu kabisa na kuwaahidi wateja wao wote na kuendelea kupata huduma bora zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya EQUITY, Isabela Maganga akizindua huduma mpya katika kituo cha huduma kwa wateja iitwayo LIVE CHAT ambayo ni kidigitali inayomuwezesha mteja kupata huduma muda wowote kwa masaa 24 kwa mwaka mzima. Huduma hiyo imeiznduliwa leo Oktoba 4,2023 katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya EQUITY, Isabela Maganga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya katika kituo cha huduma kwa wateja iitwayo LIVE CHAT ambayo ni kidigitali inayomuwezesha mteja kupata huduma muda wowote kwa masaa 24 kwa mwaka mzima. Huduma hiyo imeiznduliwa leo Oktoba 4,2023 katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.Meneja wa Benki ya Equity Tawi la Mwenge, Magreth Makundi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya katika kituo cha huduma kwa wateja iitwayo LIVE CHAT ambayo ni kidigitali inayomuwezesha mteja kupata huduma muda wowote kwa masaa 24 kwa mwaka mzima. Huduma hiyo imeiznduliwa leo Oktoba 4,2023 katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.Watumishi wa Benki ya Equity wakiwa kwenye picha ya pamoja wa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya katika kituo cha huduma kwa wateja iitwayo LIVE CHAT ambayo ni kidigitali inayomuwezesha mteja kupata huduma muda wowote kwa masaa 24 kwa mwaka mzima. Huduma hiyo imeiznduliwa leo Oktoba 4,2023 katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...