Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amepokea Hati za Utambulisho za mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kupokea nakala za hati hizo, Mhe. Waziri Makamba amemhakikishia Bw. Komatsubara kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na UNDP ili kusogeza mbele agenda yake ya maendeleo na hivyo kuinua maisha ya watanzania kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Mhe. Waziri amesema Tanzania na UNDP zimekuwa zikishirikiana kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kuwa zina lengo la kuboresha maisha ya watu kupitia maeneo ya utawala wa demokrasia, ukuaji uchumi, maendeleo endelevu mazingira endelevu na uhimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi.

Waziri Makamba ameongeza kuwa Tanzania inathmini na kutambua jitihada za UNDP katika kukabiliana na madhara yaliyotokana na janga la UVIKO 19

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNDP nchini, Bw. Komatsubara ameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza jitihada za UNDP nchini na kuongeza kuwa atakuwa sio tu Balozi mzuri wa Tanzania bali pia atakuwa mtangaza mazuri ya Tanzania kupitia kazi zake.

Bw. Komatsubara ameongeza kuwa ofisi yake ina nia ya kusaidia Tanzania kujenga uwezo kwa watu wake ili kutekeleza kwa ufanisi mipango ya maendeleo na kwamba atahakikisha UNDP inaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha ajenda ya maendeleo inafanikishwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akipeana mikono na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) baada ya kukabidhi Hati zake za Utambulisho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) katika picha na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) na ujumbe wake (kulia) katika picha na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara na ujumbe wake (kushoto) baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...