Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
GALCO Galco Insuarance Brokers ambayo ni moja ya mawakala mwakubwa wa bima Tanzania na Sehemu ya kampuni za GSM-Group wamezindua rasmi huduma ya bima ya Takaful inayosimama kama nguzo katika jamii na inasimama katika misingi ya kushirikiana pale ambapo kuwakuwa na majanga au faida.
Wakati wa uzinduzi wa bima ya Takaful uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini imeelezwa pia Galco Insuarance Brokers wana uzoefu wa miaka mitano sokoni na wameweza kutoa huduma kwa watu binafsi na kampuni nyingi zaidi.
Akizungumza leo Oktoba 5,2023 jijini Dar es Salaam Naibu Kamishna Mamlaka ya Bima Tanzania(TIRA) Dk.Khadija Said amesema bima hiyo ya Takaful inaendeshwa kwa misingi mingi ya Kiislamu kwa maana ya Sharia za Kiislam.
“Wakati wanaendesha hizi shughuli Galco Takaful watakuwa makini katika kufuata zile tararibu ambazo zinasimama katika Sharia za Kiislam lakini na taratibu ambazo tumeweka ikiwa kama ni nyezo za kutumia katika biashara hii lazima zifuatwe.
“Mamlaka imetoa kanuni za Takaful jinsi gani ya kuendesha hii bima ya kwa hiyo niwaombe Golco Takaful waitumie hii nyezo katika kufanya kazi
“Safari ya Takaful imeanza tangu mwaka 2008, nilikuwa mmoja ya wadau walioshiriki katika kuanzisha hii Takaful.”
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya GSM Group Benson Mahenya amesema katika ulimwengu ambao hakuna uhakika wa kile ambacho kitatokea mbele yetu ni lazima kujilinda na ngao inayotegemeka.
“Huduma zetu za bima sio sera tu ila ni ahadi.Ahadi ya kuwa tupo karibu nawe pale ambapo utakutana na changamoto za kibiashara na kimaisha kwa ujumla.Tunahakikisha kuwa unaweza kupitia dhoruba yoyote kwa kujiamini,”amesema Mahenya.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Biashara wa Galco Insuarance Brokers katika kampuni ya GSM Group Emmanuel Bagabu amesema huduma za bima Takafuli zinapatikana kutoka kampuni ya Galco Insuarance Brokers ambayo inashirikiana na kampuni mbalimbali ikiwemo Mayzuh Company Ltd ili kutoa mafunzo kwa wafanyakazi na kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa huduma ya Takaful.
Pia wanashirikiana na ZIC Takaful Ltd katika utoaji wa huduma hii ya bima ya kiislamu Takaful huku akieleza nia yao ni kukuza mwamvuli wao wa huduma za bima kwa watu wote kuanzia mtu mmoja mmoja , wanafamilia, wafanyabiashara, kampuni au taasisi mbalimbali ,”alisema Emanuel Bugamo meneja mkuu wa biashara .
“Wafanyakazi wetu wamepata elimu ya kutosha , wanauzoefu na wapo tayari kutoa huduma bora kwa wateja wetu,”amesema na kuongeza wao kama mawakala wa bima , bidhaa ya Takaful ni huduma inayozingatia misingi ya Kiislam .
“Wewe kama mtumiaji wa hii bima inabidi uwe na biashara zilizokuwa na uwazi na biashara zote ambazo zinazingatia misingi ya dini ya Kiislamu na sharia zake.Kama unafanya biashara ya pombe hiyo kwa kweli kwa sharia haitowezakana lakini kwa vigezo vingine vyote mtumiaji wa kawaida unapata hii bima.
“Malengo yetu ni kufikia watumiaji wa kila mkoa Tanzania na kwa watu wote ,hasa hasa tunachotakiwa ni kutoa elimu kuhusu uelewa wananchi kufahamu bima ni nini? Kuweza kuwalimisha takaful na faida zake na kuzitumia. Hivyo mpaka mwakani tunalenga kuwa na wateja wasiupungua 200 mpaka 500.
Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Bima Tanzania( TIRA) Dk.Khadija Said( wa pili kulia, ) akiwa na Mkurugenzi mkuu wa Makampuni ya GSM Group Benson Mahenya( wa pili kushoto) Mkurugenzi wa ZIC Takaful Said Basleym( wa kwanza kushoto) na mkurugenzi wa Logistic Custer Aisha Mohamed( wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua Bima ya Takaful leo Oktoba 5, 2023 jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...