Na Pamela Mollel,Arusha

Halmashauri nchini Tanzania zimetakiwa kuhakikisha inaweka mifumo mizuri inayozingatia mahitaji maalumu ya wanawake masokoni ili kuwezesha kuboresha biashara zao

Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa Asasi ya Equality for Growth Jane Mgigita wakati alipowatembelea wanawake wa soko la kilombero jijini Arusha wakiwa katika wiki ya Azaki

Amesema kuwa Arusha inaongoza kuwa na wanawake wachapakazi wanaojituma katika uzalishaji ukilinganisha na mikoa mingine hapa Tanzania

"Kupitia mradi wetu huu wa sauti ya mwanamke sokoni tumeona ukifanikiwa sana na tumeweza kufanya kazi na halmashauri zaidi ya 20 pamoja na majiji makubwa, tumeona sheria ndogo ndogo za masoko zikirekebishwa ikiwemo kuangalia mahitaji ya wanawake wa masokoni"alisema Mgigita

Amesema kuwa kupitia mradi huo wameweza kufikia mikoa 9 na wameweza kuongeza mikoa 5 na Arusha ikiwemo,hivyo nashauri wanawake kuunda vikundi ambayo vitawasaidia kukua ikiwemo kupata mikopo katika Taasisi mbalimbali za kifedha

Kwa upande wake wakili kutoka shirika la Legal service Facility Deo Bwire amesema wanawake wajasiriamali wanapata shida sana katika kupata haki zao kwa kuwa hawajui kuitafsiri sheria hasa kwa lugha ya kiswahili

"Ziara hizi za masokoni zinaleta Viongozi,wafanyabiashara pamoja kuangalia kero mbalimbali ndani ya masoko hali itakayosaidia kutatua changamoto mbalimbali zitakazojitokeza"amesema Bwire




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...