NA DENIS MLOWE, IRINGA 

MKOA wa Iringa unatarajia kuwa na kiwanja Cha kisasa Cha mchezo wa Golf kinachoendelea kujengwa na Mkwawa Golf Club katika eneo la Kihesa,  Kilolo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanja hicho Mwenyekiti wa Mkwawa Golf Club, Edmund Mkwawa alisema kuwa ujenzi wa uwanja huo utagharimu kiasi Cha milioni 200 na kutakuwa na viwanja 9 vya gofu kwenye eneo la hekta 30.

Mkwawa alisema mchezo wa Golf ni burudani inayovutia sana watalii hasa ikizingatiwa Mkoa huo ni lango kuu la utalii katika ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.

Mkwawa alisema uwanja huo licha ya kuwa na viwanja 9 kutakuwa na Hotel ambapo itaendelea kuchechemua Utalii kwa mkoa Kusini.

Alisema kuwa mchezo wa Golf unapendwa na watu wengi sana hivyo kitendo Cha kutengeneza katika viwanja wa utalii itakuwa Moja ya chafu ya kupata watalii.

Mkwawa alisema kuwa kila kitu kimekamilika kilichobaki ni ujenzi wa uwanja huo ambapo kutakuwa na kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya mchezo wa Gofu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Veronica Kessy alisema kuwa ni vyema wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutangaza vivutio hivyo vya utalii vilivyopo katika mkoani hapa  kutokana na upekee wa vivutio hivyo.

Alisema kuuwa vivutio vya Utalii ambavyo ni vizuri na vya Kipekee vinavyopatikana katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania ni fursa kwa Wananchi wa Mikoa hiyo kunufaika na kujiongezea kipato kutokana na uwepo wa vivutio hivyo.

Aliongeza kuwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa ni Moja ya maeneo yatakayovutia watalii kwani mchezo mingi huwaleta watu karibu hivyo golfu ni Mmoja ya michezo ambayo jamii ya wageni wanapenda kucheza.

Naye mbunge wa Iringa Mjini,Jesca Msambatavangu alisema uwanja huo ni chachu ya kukuza utalii Nyanda za Juu Kusini 

Aliongeza kuwa uwanja huo ambao utajengwa mkoani hapa utasaidia kukuza vipaji ya watoto katika mchezo wa Golf hivyo kuwa na Wacheza wengi zaidi hapo mbele.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy akiwa na Mwenyekiti wa Mkwawa Golf Club, Edmund Mkwawa

 

Sehemu unapoandaliwa uwanja wa Gofu wa Mkwawa Golf Club katika eneo la Kihesa Kilolo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy akiwa na Mwenyekiti wa Mkwawa Golf Club, Edmund Mkwawa na wazee wa  Iringa
Mwenyekiti wa Mkwawa Golf Club, Edmund Mkwawa akiongea
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...