Mwandishi wetu Arusha .
Wataalamu wa Wanyamapori na Maliasili katika nchi za Afrika wametakiwa kuchukua hatua madhubuti za ulinzi wa mnyama aina ya kakakuona ambao wako hatarini kutoweka.

Akizungumza jijini Arusha, mkurugenzi wa kikosi kazi cha makubaliano ya Lusaka (LATF) Edward Phiri alisema kwa sasa ‘kakakuona’ ndio aina ya wanyamapori wanaotafutwa zaidi na wafanyabiashara haramu kwa ajili ya kusafirisha kinyume cha sheria na kuwapeleka katika bara la Asia hivyo kuwaweka katika hatari ya kutoweka katika nchi za Afrika.
Phiri alisema hayo kwenye Mafunzo ya Kikanda ya Kupunguza Usafirishaji wa Wanyamapori Baharini kati ya Afrika na Asia yaliyoaandaa kwa kushirikiana na Taasisi ya Grace Farms Foundation – Marekani kwa maafisa wanyamapori kutoka Kenya, Tanzania na Cambodia
"Kakakuona tayari wametoweka katika bara la Asia na sasa wafanyabiashara wa wanyamapori wameanza kusafirisha viumbe hao kutoka Afrika na kuwapeleka huko ambako wanauawa, kwa matumizi ya kitoweo au dawa za asili ," alisema Edward Phiri.
Phiri alisema jitihada za makusudi zinahitaji katika kuokoa kizazi hicho lakini pia wanyama wengine ambao bidhaa zao zimekuwa lulu kimataifa huku vikwazo vya kimipaka vikishindwa kukamaliza tatizo.
“Mafunzo haya yanalenga kuwasaidia maafisa wetu wa mali asili na wanyama pori kutambua mbinu za kidigitali ambazo wahalifu kwa sasa wanatumia lakini pia kuwafunza umuhimu wa ushirikiano katika kushughulikia kesi hizi ili zilete matokeo chanya katika usafirishaji wa wanyama mipakani”
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Luka Kitandula alisema kuwa ipo haja kuimarisha uwezo na kukuza ushirikiano kati ya vyombo vya utekelezaji wa sheria katika swala la ujuzi kupitia kuongeza ufuatiliaji na kushirikiana kwa taarifa mbali mbali za uhalifu huu.
“uhalifu wa wanyama pori unazidi kuwa wa kisasa na wa kibunifu hivyo ujunzi huu ni muhimu kutokana na viwango vya sasa vya uhalifu wa wanyama pori katika bara letu na kuhatarisha wanyama husika kutoweka akiwemo ‘Kakakuona’” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...