Na Mwandishi wetu Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu jana Oktoba 28,2023 ametembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa maji Nzuguni na kuridhishwa na kazi inayoendelea.

Aidha amejionea maandalizi ya uchimbaji wa kisima kikubwa kitakachokuwa na urefu wa mita 300 kwenda chini kitakachochibwa eneo Nzuguni pamoja na visima vingine vya kawaida vinavyoendelea kuchimbwa katika eneo hilo.

Pia ametembelea kituo cha kuzalisha na kusukuma maji cha Mzakwe na kujionea jinsi shughuli za uzalishaji zinavyofanyika.

Prof. Katundu katika ziara hiyo ameilekeza DUWASA pamoja na Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu kuhakikisha wanapata vyanzo vingine vya maji haraka ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto ya maji katika jiji la Dodoma.

"Ninachotaka kuona Dodoma ambayo ni Makao Makuu inakuwa na maji ya kutosha, tafuteni vyanzo vingine chimbeni visima tumalize changamoto hii". amesema Prof. Katundu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...