Na Mwamvua Mwinyi, Mafia
Oct 11

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Mkoani Pwani Mwl. Kassim Ndumbo ametoa wito kwa taasisi na mashirika binafsi kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ya kijamii yakiwemo afya na elimu.

Mwl. Ndumbo ameyasema hayo wakati alipokuwa akipokea msaada wa chakula na karatasi kwa ajili ya kambi za shule za sekondari kutoka kwa Taasisi ya "Kalamu Education Foundation " (KEF).

" Ni vizuri kupata wadau wengi zaidi kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha elimu kwa kusaidia wanafunzi wetu wasome vizuri na kufaulu masomo yao" alisema Mwl. Ndumbo.

Taasisi ya KEF imetoa msaada wa unga viroba 40, mchele viroba 20, maharage viroba 12, mafuta ya kula madumu 5 na karatasi za rim 200. Msaada huu utanufaisha kambi tatu za Shule za Sekondari kwa wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya kidato cha nne mwaka huu.

Kambi zenye jumla ya wanafunzi 771 wa kidato cha nne wilayani Mafia ni pamoja na Shule za Sekondari Micheni, Kitomondo pamoja na Bweni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...