KAMPUNI ya Dough Works Limited ambao wanaendesha migahawa ya KFC-Tanzania Washeherekea Mika 10 ya kutoa huduma hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.

Katika sherehe hizo za miaka 10 pia walishiriki chakula pamoja na Watoto wenye Ulemavu kutoka kituo cha kulelea watoto wenye Walemavu Bunju cha Baba Oreste Foundation na shule ya Msingi na awali ya Rightway.

Meneja Mwendeshaji wa KFC Tanzania, Shafii Idege akizungumza na waandishi wa habari wakati wa sherehe za kutimiza miaka 10 jijini Dar es Salaam, amesema kuwa KFC Tanzania imeisaidia Serikali kupunguza changamoto ya ajira pia wanatarajia kufungua migahawa mingine miaka 10 ijayo.

"KFC imetoa huduma Miaka 10 na inaendelea kuwepo kwa miaka 10 zaidi na na mambo mazuri yanakuja". Amesema

Kwa Upande wa Mlezi wa Kituo cha Kulelea Watoto wenye Ulemavucha Bunju, amesema kuwa watoto weye ulemavu wamekuwa wakisahaurika ila KFC wamewakumbuka kupata nao chakula cha mchana hii itabioresha mahusiano mema kati ya Taasisi ya elimu na watoto wenye ulemavu.


















Matukio Mbalimbali wakati wa     KFC-Tanzania wakisheherekea Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...