Na Dkt. Noorali Jiwaji

Leo Jumamosi tarehe 28 Oktoba tutaweza kushuhudia kupatwa kwa Mwezi KIASI kwa uchache ambapo kwa lugha ya kigeni kiingereza hufahamika kama Partial lunar eclipse .

Partial lunar eclipese ni kitendo cha mwezi kupita NDANI YA kivuli cha dunia yetu ambacho hufahamika kama "Earth's Umbra and penumbral shadows" yaani ndani ya vivuli aina mbili - Yaani kivuli kilichokolea (umbra) na kivuli kilichofifia (penumbra)

KUPATWA KWA MWEZI UNAWEZA KUANGALIA KWA MACHO MOJA KWA MOJA BILA MADHARA NA HATA KWA DARUBINI BILA MADHARA YOYOTE

Iko hivi kiufupi kwa vile Jua Dunia na Mwezi vinakuwa havipo katika mstari ulionyooka kabisa kama kwenye kitendo cha total lunar eclipse (kupatwa mwezi kamilifu) ambapo utaweza kuona Jua Dunia na Mwezi vinakuwa katika mstari uliokuwa mnyoofu KABISA.

Mwezi wetu utapita katika kile kivuli cha dunia ambacho hutokea baada ya dunia kuukinga mwanga wa Jua letu , sasa upande mmoja wa mwezi utakuwa na giza au yaani kivuli kilichokolea huku upande mwengine mwezi ukiwa na mwanga wa kawaida wa rangi fulani yinayofanana na Jua la kuzama .

Maeneo mengi yataweza kuona tukio hili duniani ambapo maeneo machache ni kama vile Australia , Nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania, Nchi za Ulaya na America zote mbili Kaskazini na Kusini bila kusahau katika maeneo ya bahari za India Atlantic na Pacific. Tanzania ni katika eneo la kati kwa tukio hili kwa hiyo tunaiona katika muda muafaka.

Kwa wakazi wa Dar es salaam Tanzania tutaweza kuona tukio hilo kuanzia mida ya jioni hadi pale katika muda wa usiku mnene huku matukio mbalimbali yakiwa yanabadilika badilika hapo kwenye mwezi wetu.

Mfululizo wa matukio wakati wa Mwezi mpevu usiku wa kesho jumamosi 28 oktoba

  •   Mwezi utaanza kupatwa kimfifio saa tatu usiku (3:01 pm)

  •   Na kufikia saa nne na nusu (4:35 pm) mwezi wote utakuwa umefunikwa na kivuli mfifio.

  •   Hapo hapo saa nne na nusu (4:35 pm) kingo ya upande wa kusini

    wa mwezi kitaanza kupata uweusi.

  •   Saa tano na robo (11:14 pm) ukingo mdogo asilimia 6% utakuwa

    umeingia uweusi

  •   Baada ya hapo sehemu ya uwesi itapungua

  •   Hadi usiku wa sita kasoro (11:53 pm) uweusi wote m utatoweka

  •   Hapo kivuli mfifio kitafunika tena mwezi wote

  •   Hadi saa saba na nusu usiku wa manane (7:26 am) mwezi utakwisha

    hali ya kupatwa na kurudi tena mng’ao wa mwezi mpevu.

    ANGALIZO:
    Ni vigumu kutambua mwezi umefunikwa kwa kivuli mfifio lakini anga ikiwa wazi unaweza kutambua utofauti mdogo kati ya mng’ao wa mwezi mpevu na mwezi uliopatwa kimfifio

    PIA ANGALIA:
    Chini ya Mwezi utaona nyota moja inayong’aa sana sana. Hiyo ni Mshtarii au Sambulaa (kwa Kiingereza Jupiter) ambayo ni sayari kubwa kuliko zote na inaweza kueneza Dunia elfu moja ndani yake.

    Kwa maelezo zaidi na ya kina angalia tovuti hii:

https://www.timeanddate.com/eclipse/lunar/2023-october-28

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...