
Matukio mbalimbali siku Shampeni duniani ambayo imeadhimishwa jijini Dar es Salaam na Moët & Chandon Savoir-Faire-Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
MOËT & CHANDON Savoir-Faire-Tanzania imeadhimisha Siku ya Shampeni leo Oktoba 27, 2023 jijini Dar es Salaam pamoja na wapenzi kinywaji hicho.
Sherehe hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya MMI katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam iliangazia katika shampeni bora zaidi duniani, Moët & Chandon, inayosifika kwa utamaduni wake wa karne za utengenezaji mvinyo wa kipekee, uliojawa ufundi wa hali ya juu kutokana na umaridadi wake.
Marafiki wa Maison, wakiwa wameunganishwa na mtandao wa pamoja kwa shangwe ya shampeni, walikusanyika katika kumbi za kifahari kote barani Afrika.
Nchi nyingine wazosheherekea siku hiyo ya Shampeni ni Nigeria, Kenya, Cameroon, Ivory Coast, Afrika Kusini, ambapo kila nchi iliadhimisha siku hiyo huku wakienzi mila na ustaarabu ambao Moët & Chandon huleta katika nyakati bora zaidi za maisha.
Mmiliki wa "Style Your Soul, George Williams, ametoa mtazamo tofauti wa Kitanzania, pia amewashawishi marafiki wenye ushawishi katika tasnia na mtindo wa maisha, akihimiza sherehe ambayo inathamini nyakati zote za maisha.
"Hii ni heshima kwa kiini cha maisha, inayoakisi mvuto wa milele wa Moët & Chandon, ambao unavuka mipaka na kubadilika na kuwa mtindo wa maisha unaothamini uzuri na umoja", amesema Williams.
Katika sherehe za siku ya Shampeni watu wsalionesha umaridadi Zaidi na urembo huku wakiwa na shauku ya kuunda ushirikiano uendelevu wa mabingwa, ukichochewa na mpango wa mazingira wa Moët & Chandon," alitaja George alipokuwa atoa uzoefu wake wa moja kwa moja kutoka kwa Epernay, alipokuwa akiwachukua wageni wake.
Akizungumzia kuhusiana na namna alivyovutiwa amesema Kivutio kikuu cha ziara ya Williams ilikuwa uchunguzi wa mpango wa kilimo wa Moët & Chandon, na mpango wa mbele katika kilimo cha miti shamba, ambapo kampuni ya Moët & Chandon ilifurahia katika utuzaji wa mazingira.
Kwa Upande wa Mkuu wa Ushirikiano wa Watumiaji wa Moët Hennessy Afrika na Mashariki ya Kati, Aimee Kellen alieleza kuwa "Siku ya Champagne ni fursa ya kusherehekea urithi wetu wa kuchagiza tasnia na kushiriki juhudi endelevu Afrika na ulimwengu."
Tanzania inaungana na maadhimisho ya Siku ya Shampeni duniani kwa kujitolea kwa kufurahia, kuheshimu urithi wa Moët & Chandon, na kukumbatia mustakabali wenye uwiano na Dunia.
Mkuu wa Ushirikiano wa Watumiaji wa Moët Hennessy Afrika na Mashariki ya Kati, Aimee Kellen, alielezea, "Kwa Jumba lenye historia tajiri ya utengenezaji wa divai, Siku ya Champagne ni fursa sio tu ya kusherehekea jinsi tumeunda tasnia lakini pia kuwasiliana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...