Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Jokate Mwegelo, amesema jukumu kubwa la Jumuiya hiyo ni kuelezea mafanikio aliyoyafanya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan na kuhakikisha anapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
Akizungumza leo Oktoba 4, 2023 jijini Dar es Salaam mbele ya Wana CCM alipokuwa akichukua barua ya uteuzi baada ya kuteuliwa na Chama juzi Jokate ametumia nafasi hiyo kueleza ukubwa na nguvu ya jumuiya.
"Wanawake ni jeshi kubwa, hivyo tutasimama kuhakikisha Rais Samia anabaki katika nafasi yake na kushinda kwa kishindo, " amesema Jokate huku akisisitiza upendo na mshikamano kwa wanawake na mabinti na kuhakikisha wanasaidia katika masuala mbalimbali yenye kuleta maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Akieleza wana CCM hao, Jokate amesema kuwa na Rais mwanamke ni jambo la kujivunia na wao kama wanawake, mabinti na vijana kuwa mstari wa mbele kulinda mafanikiwa ya Rais.Mama yetu Dk.Samia anasimama kama kielelezo cha wanawake kujikomboa.
"Sasa kama amefika katika hicho kilele hatuna budi kumsaidia, kumsemea na kuhakikisha hiyo nafasi haiponyoki na sisi ndio jeshi la mama.Jeshi la wanawake litahakikisha kwenye uchaguzi zinazokuja kumuwezesha Rais Samia kushinda uchaguzi.
Akitoa salamu zake , Jokate ameishukuru Halmashauri Kuu ya Chama inayoongozwa na Mwenyekiti na Rais Dk.Samia kwa kumuona anafaa kutumika katika nafasi hiyo huku akiwaambia jumuiya hiyo nafasi hiyo ni yao.

Aidha amesema yeye ni zao la CCM na amesomeshwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uwezo wake wa kusoma umetokana na sera nzuri zilizomuwezesha kupata elimu ambayo anakwenda kuwatumikia wananchi.
Ametumia nafasi hiyo kueleza imani aliyonayo kazi yake itakuwa ni nyepesi kwani anaingia kwenye jumuiya ambayo imejipanga, imejidhatiti na kujipambanua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...