KAIMU Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha amewataka Wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe kuienzi na kushiriki katika michezo mbalimbali inayoandaliwa chuoni hapo kwani michezo ni muhimu sana kwa afya zao kwa kuwa huwaepusha na magonjwa.

Prof. Mwegoha amesema hayo katika ufunguzi wa Bonanza la michezo kwa watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe kutoka Ndaki ya Morogoro, Dar es Salaam na Mbeya yanayofanyika katika viwanja vya michezo Kampasi Kuu Morogoro ambapo amesema Menejimenti ya Chuo imeenza kufanya matengenezo ya miundombinu ya michezo ikiwa ni pamoja na kununua vifaa mbalimbali vya michezo lengo kuwawezesha watumishi kuweza kufanya michezo.

“Menejimenti ya Chuo ina maono ya muda mrefu kuhusu michezo kwa kuwa ni fursa kubwa ya kujitangaza na pia ni muhimu kwa ajili ya afya zetu, pia tutambue kuwa michezo ni ajira na utajiri, kwahiyo tuendelee kuienzi michezo ”.Alisema Prof. Mwegoha.

Kwa upande Afisa Michezo wa Chuo Kikuu Mzumbe Bw. Yohana Magongo amesema Bonanza hilo ni sehemu ya kujenga afya, pia kujiandaa na mashindano ya Shirikisho la michezo la Mashirika ya Umma na Kampuni binafasi SHIMUTA yanayotarajiwa kufanyika Jjini Dodoma hivi karibuni.

Bonanza hilo ambalo hufanyika kila mwaka likihusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, mchezo wa bao, mpira wa meza, mpira wa netiboli,mpira wa kikapu na kuhudhuriwa na Wadau wa michezo wakiwemo Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Morogoro na timu ya Moro Star kama sehemu ya kujinoa kwa mashindano yajayo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...