Na Mwandishi wetu

TAASISI ya Smart Dreamer Crowd (SDC) imetoa Elimu kwa wanafunzi wa sekondari zaidi ya mia Moja juu ya mwongozo wa kazi (Carrier Guidance) ili kuwajengea uwezo mkubwa wa ufahamu na taarifa za kotosha katika kufanya maamuzi ya maisha yao ya badae.

Akizungumzia na Michuzi blog Leo Oktoba 14, 2023 Jijini Dar es Salaam Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Smart Dreamer Crowd (SDC) Dr. Adela Syikilili amesema lengo la taasisi hiyo ni kuwasaidia wanafunzi wa sekondari ili waweze kuwa na ufahamu wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi ya mwongozo wa kazi "carrier guidance" hususani wanapofika ngazi ya Vyuo.

"Leo tulikuwa na semina nzuri sana hapa shule ya sekondari ya Wasichana Beth saida, tumeweza kuwafikia wanafunzi mia moja kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne, nia kubwa ni kutoa mwongozo wa kazi ili waweze kuwa na ufahamu mkubwa na taarifa za kotosha kabla ya kufanya machaguo mbalimbali katika maisha yao". amesema Adela

Ameongeza kuwa ndoto yao kubwa pamoja na kuwafikia wanafunzi wengi wa kitanzania haswa walio sekondari, matamanio yao pia ni kuwawezesha walimu wa sekondari nchini ili kwa kuwatumia walimu iwe njia rahisi ya kuwafikia wanafunzi wengi zaidi katika shule za Tanzania

Naye Mhadhiri msaidizi kutoka chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Fred Mkuyi amesema lengo kubwa la kutoa semina kwa wanafunzi ni kuona jinsi gani wanaweza wakafanya machaguzi ya Nini wataka wakafanye katika maisha yao kwa kuangalia yale masomo ambayo wanayasoma na matamanio yao ya badae.

"Kumekuwa na changamoto kubwa ya wanafunzi kuweza kuchagua ni 'combination' ipi aweze kusoma katika ngazi ya Elimu ya juu au kidato cha sita na badae katika vyuo vikuu, lakini kupitia SDC wanakauli mbiu ya kuweza kumsaidia mwanafunzi au mtu yeyote kujitafuta kwenye maisha kujua ni kipi ambacho moyo wake unataka ukifanye na jinsi gani anaweza akakifikia" amesema

Kwa upande wake mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya wasichana BethSaida Glory John amesema wamefarijika kwa ujio wa SDC kwa sababu tumejifunza vitu vingi, pia wamepata wasaa wa kujua 'carrier' tofauti tofauti ambazo walikuwa hawazitambui, hivyo mafunzo hayo yamewafungua katika maisha ya badae.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...