Mkurugenzi wa Fair Agro Suleiman Sharif akitoa ufafanuzi wa bidhaa za kampuni hiyo wakati wa maonesho ya Kilimo Tija Mwaka 1 Ugwachanya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Angelo Peter, mtaalamu wa biashara wa Kilimo kijijini, akitoa elimu kwa wakulima juu ya zana za kujikinga na mazao mengine ya kilimo wakati wa maonyesho ya Kilimo Tija Mwaka 1 Ugwachanya, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.


Leo, Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) limeadhimisha mwaka wa
kwanza wa mafanikio ya mradi wa USAID Feed the Future Tanzania wa Kilimo Tija katika kijiji
cha Ugwanchanya wilayani Iringa.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Bw. Peres Magiri, anayekaimu nafasi
ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Halima Dendego, wawakilishi kutoka USAID, viongozi wa
Serikali ya Tanzania, wawakilishi wa sekta binafsi na wakulima ilionesha mafanikio ya mradi
huo kwa kuwashirikisha vijana katika kilimo cha bustani chenye faida, na umuhimu wa kutumia
mbinu bora na tekinolojia pamoja na jamii kupitia ushirikiano na serikali, sekta binafsi na
mamlaka za mitaa.

“Bila msaada kutoka sekta binafsi, jumuiya za wakulima, na serikali ya Tanzania, mradi huu wa
USAID usingefanikiwa,” alisema Mratibu wa USAID Feed the Future Dk. Tor Edwards. “Ubia
wetu unalenga kusaidia biashara ndogo ndogo na za kati 2,500 za Kitanzania (MSMEs)
kuwekeza zaidi ya dola milioni 20 na kuzalisha ajira 7,400, hasa kwa vijana.”

Katika mwaka wa kwanza, mradi ulitoa ruzuku 100 zenye jumla ya TZS 727 milioni, ikiwemo
zaidi ya TZS 178 milioni kwa walengwa 22 kutoka mkoa wa Iringa. Ruzuku hizi ziliwezesha
upatikanaji wa bidhaa kama vile vifaa vya umwagiliaji kwa njia ya matone, pampu za maji, na
kreti za kuvuna ili kusaidia biashara na wakulima wadogo wa kilimo cha bustani. Kutokana na
hali hiyo, vikundi vinavyoongozwa na vijana kikiwemo Kikundi cha Agrarian cha Kilimo katika
kijiji cha Ugwachanya vimefanikiwa kufuata kanuni bora za kilimo, ambazo zimenufaisha
kikundi chao na jamii zinazowazunguka.

Lengo la mradi wa USAID Feed the Future Kilimo Tija ni kubadilisha sekta ya kilimo cha
bustani nchini Tanzania kuwa kituo chenye nguvu kikanda, kutengeneza fursa za kiuchumi na
ajira kwa vijana. 

Katika kipindi cha miaka mitano cha utendaji (2022-2027), mradi wa Kilimo
Tija wenye thamani za dola milioni 38 utalenga mikoa katika Ukanda wa Kukuza Uchumi wa
Kilimo Kusini mwa Tanzania, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. 

Lengo kuu la mradi huu
ni kuongeza fursa za kiuchumi katika mifumo ya soko la kilimo cha bustani, kwa kuzingatia
vijana, ukifanya kazi na vyama vya umma na sekta binafsi, taasisi zinazoongozwa na vijana na
wanawake, na mamlaka za serikali za kitaifa na za mitaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...