Serikali ya awamu ya sita imeendelea kutimiza ahadi ya kugawa chakula (mahindi) bure kwa wananchi waliohama kwa hiari kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Mkoani Tanga

Dhumuni la kugawa mahindi hayo kwa wananchi kila baada ya miezi mitatu (03) ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali kutoa chakula bure kwa wananchi hao kwa muda wa miezi 18 wakati wakiendelea kuzoea mazingira mapya waliyohamia kabla ya kulima na kuvuna kupitia mashamba waliyopewa na Serikali.

Katika mgao wa mwezi oktoba jumla ya gunia 1,058 zenye tani 95.22 zimegawanywa kwa kaya 529 ambapo baada ya mgao huo Wananchi hao wameendeela kuishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali katika huduma ya chakula na kuendelea kuboresha huduma za kijamii kama vituo vya afya, shule, maji, umeme, barabara, mawasiliano, posta, majosho na malambo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...