Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 5 Oktoba, 2023 ameshiriki Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola (CPC) unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana wenye dhima isemayo “The Commonwealth Charter 10 years on: Values and Principles for Parliaments to Uphold”
Katika Mkutano huo, Dkt. Tulia ameambatana na baadhi ya Wabunge akiwemo Mhe. Dkt. Alice Kaijage, Mhe. Abdallah Mwinyi, Mhe. Dkt. Pius Chaya, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu pamoja na Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi ndc
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia), akifuatilia Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola (CPC) unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana. Kutoka kwa Dkt. Tulia ni Mhe. Abdallah Mwinyi, Mhe. Dkt. Alice Kaijage na Mhe. Dkt. Pius Chaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...