MKURUGENZI  Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa, (STAMICO) Dk. Venance Mwasse ametoa mwito kwa wawekezaji kutoka ndani ya nje ya nchi kuja kuwekezaji kutokana na mazingira rafiki yanayoendelea kuwekwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Dk. Mwasse ametoa kauli hiyo leo 25 Oktoba  2023 wakati akichangia mada katika kongamano la kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania linalofanyika jijini Dar es salaam.

Amesema kutokana na jitihada zinazofanywa na Rais Samia katika kuiboresha sekta ya madini Shirika kwa sasa limejengewa uwezo  katika nyaja mbalimbali ikiwamo kuwa na Mitambo ya Kisasa ya uchorongaji wa miamba migodini.

“Kwa hiyo ninawakaribisha sana tuje tushirikiane na kila mmoja atafaidika kulingana na mazingira bora yaliyowekwa.Kwa sasa tunafanya kazi na Kampuni ya Anglogold Ashanti katika shughuli za uchorongaji wa miamba na tuna hisa katika umiliki katika mgodi mpya wa Dhahabu wa Buckreef ambao ulianzishwa mwaka jana na kwa sasa umekuwa chachu katika maendeleo ya sekta ya madini nchini,” amesema.

Tanzania ni nchi iliyojaliwa aina mbalimbali za madini ikiwamo Madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee.

Mkutano huo ni wa siku mbili na umenza leo tarehe 25 Oktoba 2023 na unalandana na Kauli mbiu isemayo “Unlocking Tanzania’s Future Mining Potential”. Kaulimbiu hiyo imelenga kuweka mazingira yatakayowezesha kuvuna madini yaliyopo Tanzania kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. 

Mkutano huu umefunguliwa rasmi  leo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk.Doto Biteko





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...