Na Mwandishi wetu, Michuzi TV
Taasisi ya GS1 Tanzania jana imefanya Mkutano Mkuu wa (12th GS1 TANZANIA AGM 2023) na ilikuwa inatimiza miaka 12 ya utendaji kazi wake.
Katika AGM ya wanaviwanda watumiaji wa Barcodes iliyofana pia ilikuwa ni AGM ya uchaguzi mkuu wa Chama cha watumiaji Barcodes nchini na iliweza kupata Bodi mpya itakayodumu kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo 2023-2026.
Wanaviwanda- (SMEs) watumiaji wa Barcode walishiriki kikamilifu katika uchaguzi ambao hatimaye uliweza kupata viongozi ambao wataendelea kutoa michango katika kuiendeleza sekta ndogo ya viwanda hapa nchini.
Katika kikao hicho ambacho kilifunguliwa na Mhe Omar Saidi Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, alieleza umuhimu wa GS1 Tanzania katika kujenga sekta ndogo ya viwanda hapa nchini, vilevile alipata nafasi ya kutoa muongozo utakaoweza kuzizatiti huduma za barcode nchini Zanzibar.
Kikao cha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 12 wa GS1 Tanzania pia kilihudhuriwa na Dr Godwill Wanga, Mkurugenzi Mtendaji wa TNBC, Eng Lugano Wilson Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akimuwakilisha Katibu Mkuu Viwanda. Taasisi nyingine zilizohudhuria ni TIRDO, EPZA, COSTECH, ZNCC, Y, EXTRATEQ, ACDI-VOCA, TIC, SMIDA, ZBS, na TBS. Viongozi
waliochaguliwa ni kama wafuatao:
Mwenyekiti wa Bodi: Eng. Benedict Lema- Tanzania Bara
Makamu Mwenyekiti: Bw. Hamad Hamad- Zanzibar
Wajumbe:
1. Bw. Khamis Issa Mohammed
2. Bi. Joyce Mapunjo
3. Bi. Eutropia James
4. Bi. Doris Emmanuel Male
5. Bw. Bassil Mwasamila
6. Bw. Ally Sechuge
7. Bw. Haruni Rashid Maarifa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...