Na Fauzia Mussa, Maelezo
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita amewataka wadau wa michezo kubuni matamasha ya michezo ya kimataifa ili kuvutia watalii.
Akizungumza na Waandishi wa habari juu ya uwepo wa tamasha la michezo la kimataifa linalotarajiwa kufanyika mwaka 2024 amesema kuzinduliwa kwa Tamasha hilo litakaloshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo tennis kutasaidia Vijana kuonyesha vipaji vyao kimataifa.
Amesema Zanzibar kuna vipaji vingi vya michezo hivyo uwepo wa Tamasha hilo kutawawezesha vijana kupata fursa ya kujitangaza kimataifa .
Aidha alisema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya michezo ikiwemo kujenga viwanja vyenye ubora ili kuweza kukidhi hadhi za kimataifa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tamasha la michezo la kitaifa ZISF Mohammed Salim Mohammed amesema Tamasha hilo lina lengo la kukuza na kuongeza fursa za uwekezaji wa utalii wa michezo ambao utalenga kuiweka Zanzibar kuwa kivutio cha utalii Duniani kote.
Amesema Tamasha la uwekezaji wa utalii wa michezo linatarajiwa Kufunguliwa Februari 08 hadi 12,2024 ambapo litajumuisha Mchezo wa baskel ,marathon ,soka ya ufukweni na tenis ya kimataifa na kushirikisha washiriki kutoka nchi mbali mbali za Afrika na nje ya Afrika.
"Katika Tamasha hili tunarajia kushirikisha Wana michezo kutoka Kenya, Uganda, Tanzania , Burundi Rwanda, Sudani ya Kusini ,Kongo, Afrika Kusini, Moroko, Misri, Algeria, Ethiopia, Zambia, Malawi,Zimbabwe na Namibia na washiriki kutoka nje ya Afrika ikiwemo Polandi,Uiengereza,Ujerumani Italia Ufaransa na Marekani." Alifahamisha Mwenyekiti ZSFI
Nae Mkurugenzi wa masoko kamisheni ya utalii Rahma sanya amesema wanaendelea kuuwaunga mkono wadau wa Michezo ya kimataifa kwani michezo hiyo ni miongoni mwa Sababu ya kuwarejesha watalii Zanzibar baada yamuda mrefu kuzowea kuja kutalii fukwe,bahari na Hali ya hewa nzuri iliopo nchini.
Hatahivyo amesema jukumu la kuutangaza utalii ni la kila mmoja hivyo Wizara inawakaribisha wadau hao ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuitangaza Zanzibar Duniani kote.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu Tamasha la michezo la kimataifa linalotarajiwa kuanza February 08, 2024.
Mwenyekiti wa Tamasha la michezo la kitaifa ZISF Mohammed Salim Mohammed akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la michezo la kimataifa linalotarajiwa kuanza February 08, 2024.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...