#Kero ya kukatika kwa mawasiliano katika Kata za Kisanga, Ulaya na Mikumi kumalizika

Kilosa - Morogoro.

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilayani Kilosa imedhamiria kumaliza kero ya muda mrefu ya kukatika kwa mawasiliano katika Kata tatu za Kisanga, Ulaya na Mikumi baada ya kukamilisha taratibu zote za ujenzi wa daraja la Mfilisi litakalokuwa na  urefu wa mita 21.75.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi rasmi kazi hiyo kwa  Mkandarasi ili aanze ujenzi, Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilosa Mhandisi Harold Sawaki amesema kuwa eneo hilo limekuwa changamoto kubwa hasa kipindi cha masika ambapo watu hushindwa kuvuka upande wa pili.

"Mto unapojaa maji mawasiliano hukatika maana kalvati lililopo ni dogo na sasa Serikali imekuja na Suluhisho la kudumu la tatizo hili".Amesema Meneja huyo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kasi yake ya kusukuma maendeleo Vijijini kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za miradi.

" Daraja hili linakuja kufungua uchumi wa wananchi na Mhe. Rais anaendelea kuleta fedha nyingi kila eneo iwe barabara, afya, elimu na maeneo mengine na wananchi nyie ni mashahidi wa hili." Amesema Mhe. Shaka.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe. Dennis Londo amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutatua kero za wananchi ikiwemo ujenzi wa barabara na madaraja katika jimbo la Mikumi.

Akiongea kwa niaba ya wananchi Bi Rehema Mlingwa ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ibegezi amesema kuwa kipindi cha masika eneo hilo huwa linasumbua  maana watu hushindwa kuvuka na hata kuvusha mazao yao na kwamba ujenzi wa Daraja hilo ni mkombozi kwao.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...