Na Andrew Chale

MAGWIJI wa muziki wa Afrika waliopata kuwika Duniani kwa nyakati tofauti Femi Anikulapo Kuti na Oliver Mutukudzi watoto wao Made Kuti wa Nigeria na Selmor Mutukudzi wa Zimbabwe ni miongoni mwa wasanii watakaopanda katika jukwaa la 21 la Sauti za Busara Februari 2024.

Kwa mujibu wa orodha mpya iliotangazwa na Busara Promotions mwezi huu wa Oktoba,2023 waandaaji wa tamasha la Sauti Busara, wametaja baadhi ya wasanii hao huku pia wakiwemo wasanii nyota wa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Sholo Mwamba, Wakazi (Dar), huku pia makundi ya The Worries of the East (Arusha), Sitti and The Band (Zanzibar),

Aidha, Wasanii wengine ni pamoja na Zoe Modiga (Afrika Kusini), Stewart Sukuma & Band Nkhuvu (Msumbiji),The Brother Moves (Afrika Kusini), Flying Bantu (Zimbabwe), Dogo Fara(Reunion), Mary Anibal (Zimbabwe), Muhonja (Kenya), Francrsco Nchukala (DRC, Zambia).

Afropentatonism (Niger, Ethiopia), Ita & Mehdy (Algeria), Aliddeki Brian (Uganda), Tamimu (Tanzania), Swahili Encouunters (Zanzibar / Various).

Mubba (Tanzania), Sibu Manai (Reunion), Lwendo Afrika (Tanzania), Anuang'a & Maasai Vocals (Kenya), Brain Boy (Zanzibar), Africulture (Tanzania) na wengine

Sauti za Busara linatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa 9 hadi Jumapili 11 Februari,2024, huku majukwaa mawili likiwemo la Ngome Kongwe, huku jukwaa la nje Forodhani ya Bustani la watu kushuhudia tamasha bure,

Aidha, tiketi za tamasha zitaanza kuuzwa mtandao wa busara kuanzia 31, Oktoba 2023, huku kukiwa na tiketi mbalimbali ikiwemo za VIP, na za kawaida ikiwemo za Watu wa ndani na Afrika Mashariki na Duniani kote.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...