Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa Kundi la Afrika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Angola Mhe. Carolina Cerqueira katika Ofisi za Spika huyo zilizopo Luanda nchini Angola leo tarehe 20 Oktoba, 2023

Pamoja na kumpongeza kwa mapokezi na maandalizi mazuri ya Mkutano wa 147 wa IPU unaotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 23 Oktoba, 2023, Viongozi hao Wamekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya Mabunge hayo.
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge Duniani kwa Kundi la Afrika (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimkabidhi zawadi ya shukrani Spika wa Bunge la Angola Mhe. Carolina Cerqueira, wakati alipomtembelea ofisini kwake Jijini Luanda, Angola leo tarehe 20 Oktoba, 2023.

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge Duniani kwa Kundi la Afrika (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifurahi jambo na Spika wa Bunge la Angola Mhe. Carolina Cerqueira, wakati alipomtembelea ofisini kwake Jijini Luanda, Angola leo tarehe 20 Oktoba, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...