NAIBU Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, ameipongeza Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) kwa kuendesha kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji inayokidhi viwango vya kimataifa.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam katika hafla ya utoaji vyeti kwa watendaji hao,iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Chande, amesema  sekta ya fedha ina wadau wengi wanaounga juhudi za serikali kutekeleza mikakati ya kisera, kisheria na kiutendaji.

“Utoaji wa elimu ya fedha kwa umma na kujenga uwezo wa wataalam wanaokidhi viwango vya kimataifa ni nguzo muhimu ya utekelezaji Mpango Mkuu wa Maendeleo ya sekta ya fedha,”“Mpango huo wa 2019/20-2029/30 wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa fedha kwaajili ya kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu,”amesema Chande.

Aidha amesema weledi na ujuzi waliopata wahitimu hao utaleta ushindani wa kimataifa katika utendaji kazi wa sekta ya masoko na mitaji nchini.“Ninaamini kwamba wahitimu wa kozi hii watashiriki kutoa ushauri na kuwezesha utoaji wa bidhaa nyingi hivyo kupanua wigo kwa wawekezaji katika masoko ya mitaji,”amesema.

Pia amesema CMSA kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Uwekezaji na Dhamana (CISI) ya London Uingereza , zimetoa wataalam wanaokidhi viwango vya kimataifa na kutoa matokeo chanya na thamani ya uwekezaji wa masoko ya mitaji kufikia trilioni 36.4.  


Naibu Waziri wa Fedha,Hamad Hassan Chande, akintunuku mhitimu cheti cha watendaji wa juu wanaokidhi viwango vya kimataifa,  anayeshuhudi ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, CPA.Nicodemus Mkama.

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji inayokidhi viwango vya kimataifa.
Mkuu wa Mipango,Ofisi ya Umoja wa Ulaya (EU),Bi Mihaela Marcu, akihutubia hafla hiyo.

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande,(katikati) akiwa katika hafla ya kutunuku vyeti wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji inayokidhi viwango vya kimataifa, Kushoto nbi Afisa amatendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA)CPA. Nicodemus Mkama, kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya CMSA Dk. John Mduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...