-1245 Lounge and Restaurant imeiwezesha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwapatia msaada wa kompyuta (Laptop).
1245 Lounge and Restaurant, Taasisi maarufu kwa sifa yake ya kuandaa vyakula na burudani nzuri, imedhihirisha dhamira yake ya kusaidia maendeleo ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kutoa msaada wa kompyuta mpakato kwenda kwa mfuko wa Utamaduni na sanaa wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Sherehe rasmi ya makabidhiano ilifanyika katika ofisi za Wizara, ikiashiria hatua kubwa ya kuimarisha rasilimali za kidijitali kwa ajili ya michezo, utamaduni na shughuli za kisanaa.
Sniper Mantana, Mkurugenzi wa taasisi ya 1245 Lounge and Restaurant, alikabidhi kompyuta hizo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, katika sherehe ambayo ilisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
"Tunafuraha kupata fursa ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na juhudi za serikali za kukuza na kuendeleza sekta nzima ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Sekta za ubunifu na utamaduni ni sehemu muhimu ya jamii yetu, na tunaamini kwamba upatikanaji wa teknolojia ni muhimu sana katika ukuaji wake.
Tunatumaini kuwa kompyuta hizi zitasaidia kuongeza uwezo wa Wizara katika kuendeleza dhamira yake na kuleta matokeo mazuri katika maisha ya Watanzania.
Kama 1245, tutaendelea kushirikiana na serikali katika kuijenga na kuiendeleza sekta hii sasa na siku za usoni” alisema Sniper Mantana kwa shauku wakati akirejelea kuhusu mchango wa kampuni.
Wakati wa kupokea mchango huo mkubwa, Naibu Waziri, Mhe. Hamis Mwinjuma alitoa shukrani zake kwa kusema: "Tunawashukuru taasisi ya 1245 Lounge and Restaurant kwa mchango wao mkubwa.
Msaada huu wa kompyuta bila shaka utaimarisha juhudi zetu za kukuza utamaduni, sanaa na michezo ndani ya Tanzania. Tunaamini zitaturahisishia kazi hasa katika kuungana na wasanii, taasisi za kitamaduni na vijana. Tunafurahi kuwa na washirika wa sekta binafsi kama vile 1245 Lounge and Restaurant ambao wanatuunga mkono katika dhamira yetu katika maendeleo ya sekta ya kitamaduni na kisanii."
Wizara ya Utamaduni, Sanaa, na Michezo ina jukumu muhimu sana katika kuhifadhi na kukuza urithi wa kitamaduni wa Tanzania, kukuza vipaji vya kisanii, na kukuza jamii inayopenda michezo. Msaada wa kompyuta uliotolewa na 1245 Lounge and Restaurant unadhihirisha utayari wao katika kuendeleza maeneo hayo muhimu, kuhakikisha kuwa yanaendelea kuimarika na kuchangia ukuaji na maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya 1245 Lounge and Restaurant, Sniper Mantana
akikabidhi kompyuta kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa, na
Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...