Na Said Mwishehe, Michuzi TV
ASASI
ya AGENDA kwa kushirikiana na Tanzania ConsumerAdvocacy and Research
(TCAR) wameitaka Serikali na madaktari wa tiba ya Kinywa na meno
kusitisha kutumia dawa yenye zebaki ya kuzoba meno yaliyotoboka kwa
makundi yanayoathirika kwa urahisi kama watoto, wanawake wajawazito na
wanaonyonesha.
Wamesema hayo wakati wa kuadhimisha Wiki ya Afrika
kupinga matumizi ya dawa yenye Zebaki ya kuziba meno yaliyotoboka huku
wakieleza kuwa Zebaki imekuwa na madhara makubwa katika afya ya
mwanadamu , hivyo ni vema ikasitishwa ili isitumike kama hatua ya
kuepusha madhara kwa jamii.
Ofisa Programu Mwandamizi wa AGENDA
Dorah Swai amesema katika kuadhimisha wiki hiyo ya kupinga matumizi ya
Zebaki katika kuziba meno wameamua kuungana ili kutoa sauti ya pamoja
ili Serikali na madaktari wa meno kuacha kutumia Zebaki.
" Wiki
ya Afrika ya kupinga matumizi ya dawa yenye zebaki ya kuziba meno
yaliyotoboka huwa inaadhimishwa kwenye wiki ya 13 - 20 Oktoba ya kila
mwaka lakini kwa mwaka huu tunaiadhimisha kuanzia Novemba 13 mpaka
Novemba 18.
"Tumelazimika kufanya hivyo Ili kuruhusu wadau
kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Tano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa
Minamata(the FiRh Conferenceof Partiesof the Minamata Conventionon
Mercury(COP5)) pamoja na kupata fursa ya kuzingatia masuala ya mkutano
huo.
" Hivyo AGENDA for Environment and Responsible Development
(AGENDA) na Tanzania ConsumerAdvocacy and Research (TCAR), pamoja na
wadau wengine tumeungana kuadhimisha wiki kama sehemu ya kuunga mkono
taasisi nyingine za kiraia zaidi ya 40 barani Afrika katika maadhimisho
ya wiki hii muhimu, "amesema Swai.
Aidha amesisitiza lengo kuu la
mwaka huu ni kuitaka serikali na nadaktari wa ya Kinywa na Meno
(Dentists)wasitishe kutumia dawa yenye zebaki ya kuzİba meno
yaliyotoboka(kwa Kiingereza DentalAmalgam) kwa makundi yanayoathİrika
kwa urahisi.
Ameongeza kwamba wanatarajia iwe hivyo pia kwa
makundi mengine siku zijazo huku akifafanua huu ni mwaka wa 10 tangu
waanze kushiriki maadhimisho hayo kuanzia yalipozinduliwa mwaka 2014.
Aidha
amesema mwito huo unaendana na matakwa ya Mkataba wa Minamata
uliopitishwa mwaka 2013 na nchi zipatazo 140 ikiwemo Tanzania, mara tu
baada ya kupitishwa, na Tanzania ikauridhia Oktoba 5, 2020.
Ameongeza
kuwa katika mkataba huo kuna marekebisho kadhaa yamefanyika likiwemo
rekebisho la watoto linalozitaka nchi wanachama kutotumia‘ Dental
Amalgam’ kwa kuzibia meno ya watoto na wanawake wajawazito na
wanaonyonyesha.
"Dental Amalgami na zebaki kwa asilimia hamsini,
inadhuru wanadamu na mazingira.Kama sehemu ya utekelezaji wa Mkataba huu
hapaTanzania Serikali imepitisha mwongozo wa pili wa utoaji hufuma za
afya ya kinywa na meno 2020 pamoja na kanuni za zebaki 2020, " ameeleza.
Ameongeza
kuwa zote hizo zinasitisha utumiaji wa 'Dental Amalgam’kwa kuziba meno
ya watoto, wanawake wajawazito na wanaonyonesha na wenye umri wa kuzaa.
Hivyo
wameitaka Serikali kukuza kasi ya usambazaji wa taarifa kwa madaktari
(sekta ya umma na binafsi)na kwa wananchi (ambao ndio walaji wa huduma
hizi).
Swai ameeleza kwamba wananchi wanahaki ya kuchagua adawa
ya kuzibia jino ila wanaweza kufanya hivyo kama watakuwana taarifa za
kutosha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TCAR Bernard
Kihiyo amesema serikali na wadau wengine wanapaswa kukuza ufahamu kwa
jamii kuhusi usitishwaji wa Dental Amalgom ili waweze kuchagua kutumia
dawa zisizo na zebaki.
Pia amesema Serikali inatakiwa isitishe
matumizi ya Dental Amalgam kwa watu wa makundi mengine ambayo
hayajaguswa kwa sasa kama wanawake na wanaume wengine ili makundi yote
ya wananchi yaguswe kama vile ilivyofanya nchi ya Garbon ambayo kwa
mwaka huu imepitisha kusitishwa kwa Dental Amalgam kwa watu wote.
Awali
Katibu Mtendaji wa AGENDA Haji Rehani ameeleza kwamba utumiaji wa dawa
zisizo na zebaki kwa kuziba meno yaliyotoboka inawezekana kabisa —
nazimekuwazinatumikahata kablaya kupitishwa kwa Mkatabawa Minamata ..
Amesema
baadhi ya dawa za kuziba meno ambazo hazina zebaki ambazo pia zimekuwa
zinatumika hapaTanzania huku akifafanua ni Zebaki ni sumu ya mfumo wa
fahamu ambayo inaweza kuathiri ubongo na mfumo wa neva wa binadamu.
"Tunaweza
kutoka kwa mama na kuingia kwa mtoto akiwa tumboni au kupitia maziwa ya
mama wakati wa kunyonyesha.Athari nyingine za zebaki ni kutetemeka
mwili, ku fubaza uwezo wa kuona na kusikia,kupooza kwa viungo.
"Pia
kukosa usingizi na kuongeza kuwa na hasira. Pia zebaki inaweza kuathiri
mfumo wa uzazi, inaweza kuathiri mbegu za kiume, madhara wakati wa
kuzaliwa mtoto, mimba kutokana matatizo mengine ya kujifungua."
Ofisa Programu Mwandamizi wa AGENDA Dorah Swai (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wakiadhimisha Wiki ya Afrika ya kupinga matumizi ya dawa zenye zebaki ya kuziba meno yaliyotoboka.Kushoto ni katibu Mtendaji wa AGENDA Haji Rehani na Mkurugenzi Mtendaji wa TCAR Bernard Kihiyo(kulia).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...