Na Ashrack Miraji Same kilimanjaro
MBUNGE wa Same Magharibi Dk.David Mathayo amesema michezo inawajenga vijana kuwa na mahusiano mazuri Katika nyanja mbali mbali na kuweza kutimiza ndoto zao pia kuachana na vitendo viovu kama ukabaji na kutumia madawa ya kulevya, bangi na mirungi
Hayo ameyasema wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa Michuzi Blog kuelekea uzinduzi wa Dk.Mathayo Cup inayotarajia kuanza Novemba 26 katika jimbo la Same Magharibi mkoani kilimanjaro ambapo timu 56 zitakwenda kushiriki mashindo hayo.
Amesema dhamira yake kwa vijana ni kubwa kwani anatamani kuona wanafika mbali na kutimiza ndoto zao hivyo atakuwa nao bega kwa bega katika kuleta maendeleo chanja kwenye jimbo la Same Magharibi sambamba na kuza vipaji vyao.
Dkt Mathayo amesema pia michuano ya Mathayo Cup ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk.Rais Suluhu katika sekta za michezo huku akisisitiza wanaona Rais akifatilia michezo tofauti kwa ukaribu na kuzipa timu zetu hamasa katika mashindano ya kimataifa.
"Mimi kama mwakilishi wake katika Jimbo la Same Magharibi nitahakikisha vijana wa Same Magharibi wananufaika katika michezo na shughuli mbalimbali za kiuchumi, " amesema.
Aidha ametumia nafasi hiyo kueleza mambo makubwa ambayo Rais Samia ameyafanya katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa miundombinu katika sekta ya afya, barabara, elimu pamoja na kuboresha maeneo mengine kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
"Niwaombe wananchi wa Jimbo langu kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwenye jimbo letu na Taifa."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...