Njombe
Ditrick Muogofi (43) wa kesi ya mauaji No 53 ya mwaka 2023 amehukumiwa kunyogwa hadi kufa kutokana na kosa la mauaji aliyoyatekeleza katika kijiji cha Itulike kata ya Ramadhani mjini Njombe.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamod Hassan Banga ameweka wazi juu ya hukumu hiyo wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Oparasheni mbalimbali za Polisi mkoa wa Njombe kwa kipindi cha kuanzia September 1 mpaka October 31,2023 ambapo pia amesema katika kipindi hicho Alex Simon Gwavi (65) akihukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa kike huko Mundindi katika wilaya ya Ludewa.
"Ditrick Muogofi huyu alihukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la maujai huko katika kijiji cha Itulike,Ramadhani Njombe lakini kuna mtu anaitwa Alex Simon alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka binti yake katika kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa kwa kesi namba 44 ya mwaka 2023"amesema Kamanda Banga
Aidha amesema licha ya mafanikio makubwa waliyoyapata katika kipindi hicho lakini pia wameweza kuwakamata watuhumiwa 163 kwa tuhuma mbali mbali ikiwemo za wizi wa Bajaji na Pikipiki,uporaji,uvunjaji pamoja na mauaji ambapo pia wamekamata vielelezo mbalimbali zikiwemo Bajaji nane.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...