Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mwenyeki Ndugu Shemsa Mohamed imeridhishwa na utekelezaji wa miradi Wilayani Bariadi kufuatia ziara iiliyofanyika Novemba 25,2023 ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambapo baadhi ya miradi iliyokaguliwa ni pamoja Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi ya Mlimani yenye thamani ya shilingi 540 milioni iliyopo katika Kijiiji cha Sengerema, kata ya Dutwa na mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa yenye thamani ya shilingi 4 Bilioni iliyopo Kijiji cha Igegu, kata ya Sapiwi na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

Kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kuiomba serikali kuhakikisha wanamaliza kwa muda uliopangwa huku ubora na ufanisi wa miradi hiyo ukizingatiwa

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Nawanda ameishukuru kamati hiyo kwa ukaguzi na miradi huku akiahidi kushughulia na kufuatilia maagizo yote yaliyotolewa na kamati hiyo yenye lengo la kuhakikisha miradi inakuwa bora na imara zaidi.

Kamati ya Siasa Mkoa wa simiyu imeendelea na ziara yake katika Wilaya ya kukagua utekelezaji wa ilani kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa na ambayo imeshatekelezwa.

“Kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu inakupongeza Mheshimiwa Dkt Yahaya Nawanda Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mheshimiwa Simon Simalenga na timu yote ya Wataalamu wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa Miradi inayotokana na Fedha zilizoletwa na Serikali ya Mama yetu Samia Suluhu Hassan, sisi Chama cha Mapinduzi tumeridhishwa na Ubora wa Miradi unaotokana na usimamizi wenu makini” Alisema Mwenyekiti Shemsa Mohammed






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...