CHUO cha Ustawi Ustawi wa Jamii Kinashiriki Uzinduzi wa zoezi Kusikiliza Kero za Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Hasa kwa Wananchi wa Wilaya ya Kinondoni. Uzinduzi unaofanyika katika viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe, Dar es Salaam.
Uzinduzi wa zoezi la kusikiliza Kero za Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam unaratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kushirikisha Taasisi mbali mbali za serikali zinazotoa huduma kwa Wananchi.
Chuo cha Ustawi wa Jamii kupitia Kituo chake cha Elimu, Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia kinatoa huduma mbali mbali kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika zoezi hili.
Zoezi hili la kusikiliza na kutatua kero za wananchi linafanyika kwa siku mbili, leo tarehe 04/11/2023 mpaka tarehe 05/11/2023. Zoezi hili ni endelevu ambapo litafanyika sehemu mbali mbali za mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa upande wa Nazari Sanga kutoka Kinondoni ameshukuru kwa kupewa huduma baada ya kukutana na Maafisa wa Ustawi wa Jamii na kuweza kutatua kero yake.
"Nashukuru nimekutana na watu wa Ustawi wa Jamii nilikuwa na tatizo la kudhulumiwa nyumba nimepata majibu mazuri namshukuru Mkuu wa mkoa kwa siku hii ya kusikiliza kero za sisi wanyonge", amesema

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...