Na Mwandishi wetu, Arusha
MAMLAKA
ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) imeitaka jamii kujihadhari na
upatu haramu kwani ni hatari kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Meneja
uhusiano wa CMSA Charles Shirima ameyasema hayo jijini Arusha
akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa.
Shirima
amesema jamii ijihadhari na matapeli wanaoahidi watu kuvuna pesa nyingi
kirahisi hivyo waepuke kupoteza pesa ya jasho lao kupitia upatu haramu.
"Kutokana
na hali hiyo watanzania wanapaswa kujiinga kwenye masoko ya mitaji
kwani ni sehemu ya mfumo wa sekta ya fedha unaowezesha upatikanaji wa
fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo ya muda mrefu yaani
mwaka mmoja," amesema
Amesema fedha za maendeleo hupatikani kwa kuuza hisa za kampuni, hatifungani za kampuni na vipande katika uwekezaji wa pamoja.
Mchambuzi
fedha mwandamizi wa CMCA, Witness Gowelle amesema kupitia maadhimisho
hayo wametoa elimu kwa wajasiriamali mbalimbali ili kuwajengea uwezo
zaidi.
"Elimu mbalimbali
tuliyotoa kwa wajasiriamali watanufaika nao kupitia masoko ya mitaji ili
kujiepusha na upatu haramu," amesema Gowelle.
Mjasiriamali
wa kutoka wilayani Ngorongoro, Sas Kotete amesema wajasiriamali wengi
wameathirika kupitia upatu haramu hivyo elimu waliyoipata kutoka CMSA
itawasaidia kuepuka hayo.
Mjasiriamali
mwingine wa mkoani Arusha, Naini Losusu ameipongeza CMSA kwa kuwapa
elimu hiyo kwani inawajengea uwezo zaidi juu ya upatu haramu
Maadhimisho
ya wiki ya huduma za fedha kitaifa kupitia kauli mbiu ya elimu ya
fedha, msingi wa maendeleo ya uchumi, yanafanyika jijini Arusha, kwa
siku sita kuanzia Novemba 20 hadi 26 mwaka huu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kufungua rasmi maadhimisho hayo Novemba 22 jijini Arusha ,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...