Tarehe 24 Novemba, 2023 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Nnauye amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa jimboni humo.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu lililopo katika kata ya Mtua ambapo litaondoa tatizo kubwa lililopo katika eneo hilo la wananchi kuliwa na mamba mara wanapo pita katika eneo hilo.

Miradi mingine aliyokagua Mbunge Nape ni pamoja na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami inayopita katika Kata za Nyengedi, Mnara, Rutamba na Rondo; Mradi wa maji safi wenye thamani ya zaidi ya TZS 2.6 uliopo katika Kata ya Manara Rondo na ujenzi wa barabara ya changarawe katika kata ya mnolela kijiji cha Simana.

Mbunge Nape amefanya ziara hiyo fupi ili kukagua maendeleo ya miradi hiyo kwa lengo la kuwezesha umalizikaji wake kwa wakati.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...