Mkuu wa Wilaya ya Ludewa- Victoria Mwanziva amefanya ziara ya kutembelea Gereza la Wilaya Ludewa.

Akizungumza na viongozi mbalimbali amesema “Gereza hili lipo chini ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA)- likizalisha Wastani wa mavuno wa zaidi ya Tani 520 kwa mwaka- Gereza hili linatekeleza mradi wa Kilimo likiwa na lengo la kuzalisha chakula cha kutosheleza kuhudumia Gereza hili na magereza mengine chini ya mradi huu wa SHIMA kwa Mkoa wa Njombe, na kitaifa”

Katika hatua nyingine amepongeza mpango uliopo wa wafungwa kupatiwa ujuzi na stadi za kazi zitakazo wasaidia wanaporejea uraini na kusisitiza utaratibu huu uendelee.

Mwisho DC Ludewa amewashika mkono Magereza Ludewa kwa kuwapatia mahitaji muhimu mbalimbali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...