Na Mwandishi Wetu, Mpwapwa

MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Sophia Kizigo amemshauri Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu Dk.Doroth Gwajima kama inawezekana iwepo sheria ambayo mtu akikamatwa kaajiri mtoto kufanya kazi za ndani atoze faini.

Akizungumza wakati akitoa ushauri huo Mkuu wa Wilaya Kizigo amesema kwa sasa kuna wimbi kubwa la watoto waliomaliza darasa la saba kutoka vijijini kwenda kwenye miji kama Dar es Salaam kuwa ma house girl huku akifafanua kuna mawakala wanaounganisha hao watoto na wanaopenda kufanya kazi.

“Nimemshauri Dk.Waziri Gwajima kama inawezekana iwepo sheria ambayo mtu akikamatwa kaajiri mtoto atozwe faini.Lakini iwe shirikishi katika jamii atakayetoa taarifa ya mtu aliyeajiri mtoto basi apewe sehemu ya fedha ya faini atakayotozwa mhusika.”

Akifafanua zaidi wakati anatoa ushauri huo Mkuu wa wilaya ya Mhe.Kizigo  amesema kupitia vyombo vya habari angependa kumshauri Waziri Dk.Gwajima kama inawezekana iwekwe sheria kali shirikishi itakayosaidia watoto sio wa Mpwapwa peke yake bali nchi nzima wasiendelee kutumikishwa kufanya kazi za nyumbani kabla ya umri wa kufanya kazi haujafika

“Kwasababu wale watoto wako chini ya umri wa miaka 18, Waziri anaweza akafanyaje ,nitoe mfano labda sheria wanaweza kuweka faini kwa mtu yoyote atakayekutwa ameajiri mtoto chini ya miaka 18 atatakiwa kulipa faini Sh.200,000 na msamaria atayakayetoa taarifa ya mtoto kutumikishwa kwenye nyumba fulani atapewa Sh.100,000 kutoka kwenye hiyo faini.

“Maana yake tutapata taarifa moja kwa moja na kunaweza kuwa na namba maalum ambayo mtu atapiga kutoa taarifa ya mtoto chini ya miaka 18 anatumikishwa na kwa kufanya hivyo kutakuwa na taarifa nyingi.

“Kuliko kutegemea mtoto apigwe kama yule anayezunguka mtandaoni anaomba kufikishwa nyumbani kwao. Kwa kweli hali ni mbaya na binfasi nisingependa kuona mtoto yoyote anatumikishwa kwenye umri mdogo badala ya kwenda kusoma,”amesema.

Ameongeza kuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amepeleka fedha nyngi kwa ajili ya miradi na wananchi wa Mpwapwa ni mashahidi.“Rais Samia amejenga shule nyingi za kidato cha kwanza mpaka cha nne ili watoto wasome sio wasio waende kuwa ma- house girl.

“Kwa hiyo Waziri Gwajima anaweza kufanya hilo , wanaweza kuweka hata faini Sh.milioni tano kwa mtu anayetumikisha mtoto lakini anayetoa taarifa atapewa Sh.milioni tatu, tukifanya hivyo  naamini hakuna atayetumikisha mtoto kwasababu watu watatoa taarifa.”







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...