Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ilembo Kata ya Mpui kwa ajili ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa Kijiji cha Ilembo na aliyekua Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndugu Lucas Kasanya.

Katika mkutano huo wananchi wamedai Mwenyekiti huyo wa zamani na mwenzake Herman wamehodhi ekari 130 Mali ya Kijiji kwa manufaa yao wamekua wakikodisha kwa lengo la kujipatia fedha.

Pia wananchi walitoa ufafanuzi kuwa mashamba hayo ni mali ya kijiji ambapo awali yalikua yanalimwa na kijiji na mazao yaliyopatikana yalitumika kwa shughuli za maendeleo na baadae baadhi ya wananchi waligaiwa ekari mbili mbili kwa ajili kulima mazao ya chakula.

Katika mkutano huo,wananchi walimueleza Mkuu wa Wilaya kwamba Lucas Kasanya alihamia kijijini hapo kutoka Tanga na baadae aligombea nafasi ya mwenyekiti wa Kijiji Cha Ilembo, alitumia njia za kilaghai akishirikiana na Bwana Herman kutwaa maeneo hayo.

Baada ya kusikiliza pande zote za mgogoro iliamuliwa kwamba shamba hili lirejeshwe Kwa mmliki wa awali ambaye ni Serikali ya Kijiji na Mkurugenzi asimamie kupanga matumizi ya shamba hili ili litumike kwa manufaa ya kijiji na pande zote za mgogoro zimeridhia maamuzi haya.

Wananchi wamempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu kijijini hapo.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...