NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SERIKALI
kupitia Mfuko wa Fidia kwa Wafanmyakazi (WCF) imetangaza Fao jipya la Huduma ya
Utengemao wa Kijamii (Social Rehabilitation) kwa wafanyakazi wanaopata ulemavu na magonjwa
yatokanayo na kazi na hivyo litawaongezea faraja, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amesema.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023, alipokutana na wanufaika wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani inayotarajiwa kufanyika kitaifa jijini Dodoma, Desemba 2, 2023, amesema “Ndugu zangu hivi karibuni tutaanza kutoa Fao la Huduma ya Utengamao wa Kijamii na kutoa mafunzo ya kujenga ujuzi kwa wafanyakazi wanaopata ulemavu wakiwa kazini na aina ya ujuzi tutakaotoa utategemea uhitaji.” Alisema
Alisema
lengo la Serikali ni kumpatia mfanyakazi ujuzi ambao utaendana na hali ya ulemavu wake,
mfano alikuwa dereva na akapata ajali iliyopelekea ulemavu wa miguu, huyu anaweza kubadilisha ujuzi na kusomea kazi nyingine.
Sambamba
na kuwajengea ujuzi, fao hilo pia litatoa fursa ya kumjengea miundombinu inayoendana
na hali yake, na hivyo kumuwezesha kumudu maisha katika mazingira
anayoishi.” Alifafanua Profesa Ndalichako.
Kwa
upande wao, wanufaika wa WCF wameishukuru Serikali kwa huduma wanazopokea
kutoka katika Mfuko huo licha ya kupata ulemavu na wengine kuondokewa na
wapendwa wao.
“Naomba
kuhamasisha waajiri kuweza kuwachangia wafanyakazi wao, kwani viwango vya
uchangiaji ni vidogo, tunaishukuru Serikali imepunguza viwango vya uchangiaji
hadi kufikia asilimia 0.5” Alisema Norbert Tesha, ambaye
amepata ulemavu wa kudumu baada ya kupata ajali akiwa kazini mwaka 2016.
“Hatuwezi
kujua kesho yetu, lakini kama kuna misingi mizuri iliyowekwa leo, basi kesho
yetu itakuwa njema, kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.” Alisema, Bw. Tesha.
Mnufaika mwingine Bi. Emmaculet Nhigula, ambaye alimpoteza mumewe kwa ajali ya gari, amesema, “Mimi na watoto wangu wanne, tunanufaika sana na Mfuko huu, rafiki yetu kwa sasa ni WCF, huwa nikipita kwenye barabra hii na kuliona jengo lenu, ninasema hawa ni rafiki zangu wanaotembea na mimi nyakazi ngumu." Alisema
Alisema yale mafao ya kila mwezi yamekuwa na msaada
mkubwa sana, yamesaidia kusomesha watoto wangu na sikuweza kuwahamisha kutoka
shule walizokuwa wanasoma kabla ya kufariki baba yao.” Alisema Bi. Emaculate.
Maadhimisho
ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu, yanalenga kuwahamasisha viongozi wa
taasisi za kibiashara Duniani kutambua mchango maridhawa wa watu wenye ulemavu.
Kwamujibu
wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwasasa inakadiriwa kuwa watu bilioni 1.3
duniani wanaishi na changamoto ya ulemavu, hii ni sawa na asilimia 16% ya Watu
wote duniani.
Kauli
mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “ Tuungane katika hatua za Kuokoa na
kufikia Malengo ya SDGs kwa Watu wenye Ulemavu”.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (wapili
kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt.
John Mduma (wakwanza kushoto), wakati akizungumza na wanufaika wa Fidia
inayotolewa na WCF, kwenye Ofisi za Mfuko huo, jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...