BODI ya Filamu Tanzania imetazitaja Filamu 57 zilizopita katika mchujo wa pili wa zilizofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha tuzo huku wasanii waliokosa sifa kuingia katika kinyang’anyiro hicho wakumbushwa kutengeneza kazi zenye ubora zaidi.

Akitangaza mchujo wa kazi zilizopita Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo amesema filamu zilizopita ni zile zilizokidhi vigezo na ubora unaotakiwa na kwa jopo la majaji limechukua filamu chache zenye ubora zaidi.

Hatua hiyo imekuja baada ya jopo la majaji kuchambua filamu zilizopita mchujo wa awali, ambapo zilikuwa ni 204 kati ya filamu 565 zilizopokelewa.

“Tunatoa rai kwa wadau na mashabiki wa filamu kuendelea kufuatilia muendelezo wa tamasha la Tuzo za Filamu 2023 kwenye mitandao ya kijamii na kuwapigia kura waliofanikiwa."

Pia Kiagho ametangaza rasmi kuwa kilele cha tuzo za filamu zitafanyika Desemba 16, mwaka huu ukumbi wa Superdom Masaki Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki jumla ya filamu 30 ziliwasilishwa ambapo 10 zimefaulu na kati ya hizo tano zikiwa katika kipengele cha filamu bora fupi na tano ndefu.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ameipongeza bodi hiyo kwa kuendelea kuwalea na kuwapa wasanii miongozo mizuri hadi kufikia hatua hiyo.

Pia ametoa wito kwa Viongozi wa Mashirikisho yote ya Sanaa kuamka na kuendana na Kasi ya Kiburudani zaidi bandika bandua kwa matukio mbalimbali yenye kuongeza ajira na kuzalisha kipato kwa wasanii nchini.

Amesema wasanii ambao kazi zao hazikufanikiwa kuingia hatua hii ya pili wasikate tamaa bali wajipange upya kwa ajili ya mwakani huku pia, amewapongeza wadau mbalimbali wakiwemo wadhamini waliojitokeza kuunga mkono tuzo hizo.

Nae Msanii na mtayarishaji wa kazi za filamu Chuchu Hansy amesema mwaka 2023 umekuwa mzuri kwake kutokana na filamu yake "Jeraha" kuingia katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo kwa vipengele vitano ikiwemo Msanii bora wakike Mariam Ismail kutoka filamu ya hiyo,tamthilia bora ya mwaka ,mchezaji bora mwenza ambae ni Single Mtambalike, Muziki bora ,Msanii bora chaguo la watazamaji Mariam Ismail pamoja na Ubunifu na usanifu bora (Graphics).

"Naomba watanzania ukifika wakati wa kupiga kura waipigie Tamthilia ya jeraha ambayo imekuwa tamthilia bora iliyosisimua na kufundisha watanzania wengi."

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa akizungumza na Wanahabari  na Wadau wa Filamu mara baada ya kutangazwa rasmi kwa mchujo wa pili wa Filamu zilizoingia katika kinyang'anyiro cha Tuzo za Filamu 2023 ambapo zinatarajiwa Kufanyika  Disemba 16,2023 ukumbi wa Superdom Masaki Jijini Dar es Salaam
 

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo akizitaja Filamu zilizofanikiwa kupita kwenye mchujo huku akiwasisitiza wasanii kuendelea kufanya kazi zenye ubora na viwango zaidi ili zilete ushindani katika soko la kimataifa
 

Chuchu Hansy,Joti ni miongoni mwa Wasanii  waliohudhuria katika hafla ya kutangazwa kwa Filamu 57 zilizopita mchujo wa pili kuelekea kilele cha usiku wa tuzo za Filamu  zitakazofanyika Disemba 16,2023 Ukumbi wa Superdom Masaki Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...