NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Halmashauri ya Mwanga imeandaa andiko lenye thamani ya Sh.bilioni 3.2 na kuliwasilisha Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya kisasa wilayani humo.
Mhe Dkt. Dugange ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha sita mkutano wa 13 unaoendelea jijini Dodoma.
" Mhe Spika Serikali inatambua ufinyu wa stendi ya magari katika Halmashauri ya Mwanga lakini tayari Ofisi ya Rais-TAMISEMI tumepokea andiko lenye thamani ya Sh. bilioni 3.2 tokea Agosti mwaka huu na hatua iliyopo hivi sasa ni ya watalaamu wetu wizarani kuendelea na mapitio ya andiko hilo kulingana na vigezo," amesema Dkt. Dugange.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...