Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima ametoa wito kwa waajiri wa Maafisa Maendeleo ya Jamii kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu, Mashirika ya Umma, Taasisi za Elimu, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Taasisi nyingine zote kuwawezesha wataalamu hao kushiriki kongamano la wataalamu wa Maendeleo ya Jamii 2023.

Kongamano hilo litafanyika Novemba 20- 22, 2023 na litakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru likitarajawa kushirikisha jumla ya washiriki 1500 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watashiriki kongamano wakiwemo kutoka; Sekretarieti na Mamlaka za Serikali za Mitaa; Serikali Kuu; Mamlaka mbalimbali za Serikali; Vyuo na Taasisi za elimu ya Juu; Mashirikia yasiyo ya Kiserikali; Mashirika ya kimataifa; Mashirika ya dini; Mabonde ya Maji; Majeshi; Taasisi za kifedha na Sekta binafsi.

Akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea Kongamano hilo leo Novemba 6,2023 Jijini Dodoma Dkt.Gwajima amesema ada ya ushiriki shilingi 350,000/=.

"Nitoe rai kwa waajiri wa Maafisa Maendeleo ya Jamii kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu, Mashirika ya Umma, Taasisi za Elimu, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Taasisi nyingine zote kuwawezesha wataalamu hao kushiriki kongamano la wataalamu wa Maendeleo ya Jamii 2023.,"amesema Gwajima

Dkt.Gwajima amesema, lengo kuu la kongamano ni kutoa fursa ya wataalamu kujadiliana juu ya mchango wa sekta ya maendeleo ya jamii na changamoto kwenye maendeleo ya taifa pamoja na kuendelea kubuni mbinu za kutekeleza mipango ya Serikali ya awamu ya sita katika kuwezesha wananchi kujiletea maendeleo endelevu kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka. Kaulimbiu ya kongamano hili ni “Sekta ya Maendeleo ya Jamii: Msingi Imara wa Uwezeshaji wa Wananchi.”

"Kulekea maadhimisho hayo, shughuli mbalimbali zinatarajiwa kufanyika kama vile; Mkutano Mkuu wa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Sekretarieti na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mkutano wa Chama cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii, Maonesho ya shughuli za Maendeleo ya Jamii, Maonesho ya Taasisi na Vyuo vinavyotoa fani ya Maendeleo ya Jamii na Mijadala ya kitaaluma,"

Na kuongeza kuwa "shughuli nyingine muhimu itakayofanyika katika kilele cha maadhiimisho ya miaka 60 ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ni uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana ( Girls' Hostel) lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 568 na kumbi pacha za mihadhara ( twin lecture theatre) yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1008 kwa pamoja. Mradi huu uliogharimu shilingi bilioni 4.8 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan umekamilika na tayari umeanza kutumika," ameeleza Gwajima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...