Vero Ignatus Arusha
Maadhimisho Siku ya Mtoto duniani yaliyotokana na mkataba wa kimataifa wa Haki za mtoto ya mwaka 1989,ambapo nchi ya Tanzania iliridhia kulindwa kwa za haki watoto sambamba na kuwasaidia namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Hayo yamesemwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewataka washauri elekezi wa mazingira kujikita kwenye Kumjengea mtoto uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwani chakula kinapokosekana watoto ndiyo wanaoathirika zaidi
Ametoa wito huo leo Jijini Arusha katika siku ya mtoto duniani na huku akisema Jabo la kuwalimda watoto na kutunza mazingira ni suala ambalo halina majadala Lazima tulipe kipaumbele
Akizungumza katika siku hiyo ya Mtoto duniani Mkuu wa Idara ya mtoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastiani Kitiku alisema siku hiyo wanajadili juu ya
Mabadiliko ya tabia nchi na watoto na namna ya kulinda mtoto sambamba na
Kujaribu kukumbushana umuhimu wa hali za watoto
Kitiku ameainisha haki tano za watoto ikiwa ni pamoja na kutunza haki za watoto didhi ya ukatili,haki ya Kuishi kuendelezwa ,kulindwa ,kushiriki nakushirikishwa katika masuala yanayowahusu pamoja na kuhakikisha hawabaguliwi kwa haki yeyote ile.
Akitoa salam za mkoa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha , mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda amesema watoto ni 50% ya watanzania wote hivyo ameishikuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii na UNICEF kuchagua mkoa huo kwaajili ya kufanyika maadhimisho hayo na amewahakikishia kuwa mkoa upo shwari salama na timamu
Kwa upande wake muwakilishi Mkazi Unicef Tanzania Bi Elk Wisch amesema kuwa kizazi hiki watoto chipukizi jamii inahitajika kuwaweka katika shughuli wanazozifanya ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Wisch amesisitiza kuwa lazima Watoto,vijana balehe wafundishwe kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kuepuka kuwapoteza wanyama waliopo hatarini kupotea, hiyo itajenga maana halisi ya Kauli mbiu ya siku ya mtoto Duniani.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na amesema kuwa Maadhimisho hayo kwa nchi ya Tanzania yamefanyika leo tarehe 22/11badala ya novemba 20 kutokana na mwingiliano wa majukumu huku akiendelea kusisitiza kulindwa kwa haki za watoto nanamna ya kuwafunza kukabikiana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha Mpanju amesisitiza kuwa kaulimbiu hiyo ni dhahiri imekuja kwa wakati muafaka kwaajili ya kuwasaidia watoto wetu kutambua na kuwapatia elimu ya kutosha ili waweze mabalozi wazuri wa kukabiliana na mabadiliko hayo kwani serikali inaratibu na kusimamia haki zote za watoto ikiwemo haki ya kuishi na kumlinda didhi ya vitendo vyote vya ukatili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...